Naibu Waziri wa Madini, Dkt Steven Kiruswa akishuhudia Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini Tanzania, STAMICO, Dkt. Venance Mwasse (kushoto) akibadilishana hati na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ABSA Commodities ya Uswisi, Bw.Gerges Schmickrath baada ya kutiliana saini mkataba wa miaka 5 ya uchimbaji makaa ya mawe mkoani Songwe.
Wakitiliana saini mkataba
Waandishi wa habari na watumishi wa Stamico
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Drumlin, Linusi Seushy mtanzania ambaye ameingia mkataba na ABSA kusafirisha makaa ya mawe kutoka kwenye machimbo Kiwira mkoani Songwe hadi Bandari ya Mtwara kwa kutumia malori yake 3000. Kampuni hiyo itaajiri madereva 600 kwa kila lori wawili.
Seushy amesema kuwa wamejiandaa kuhakikisha kila kitu kinafanyika kama kilivyopangwa kwakuwa ni jambo la kihistoria kwa nchi.
Wakionesha mkataba
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ABSA Commodities, Gerges Schmickrath akipongezana na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo, Walter Nyaki
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ABSA Commodities, Gerges Schmickrath akipongezana na Seushy
Gheorghe Stan na Walter Nyaki wa Kampuni ya ABSA wakiwa na furaha
Naibu Waziri Kiruswa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa STAMICO, ABSA, Drumlin na wa wizara ya madini.
Naibu Waziri Kiruswa akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ABSA Commodities, Gerges Schmickrath.
Naibu Waziri Kiruswa akiagana na Seushy
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video ujue yaliyojiri wakati wa hafla hiyo....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDAMHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇