Idadi ya Sekondari ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini (Kata 21), hadi leo hii, ni kama ifuatavyo:
*Sekondari za Kata/Serikali: 22
*Sekondari Binafsi: 2
*Sekondari mpya zinazojengwa: 10
*High Schools: 1
(Masomo ya Arts)
UJENZI WA HIGH SCHOOLS za Masomo ya Sayansi unaendelea kwa kujenga miundombinu ifuatayo:
Maabara (Laboratories)
Sekondari zote ndani ya Jimbo letu zinakamilisha majengo ya maabara 3 (physics, chemistry na biology) na miundombinu yake.
Mabweni (Domitories)
Ujenzi wa mabweni ya Wanafunzi wa Kidato cha V & VI unaendelea kwa baadhi ya Sekondari.
Bwalo la Chakula (Dinning Hall)
Sekondari inayohitaji kuwa na High School italazimika kujenga Bwalo la Chakula kwa Wanafunzi hao.
Wanakijiji wa Kata ya Kiriba wameamua kujenga High School ya masomo ya Sayansi wakiwa na malengo ya kuanza kupokea Wanafunzi wa Kidato cha V ifikapo JULAI 2022
Tafadhali sikiliza CLIP kutoka RADIO Efm kuhusu ujenzi wa Kiriba High School - imeambatanishwa hapa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇