LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 22, 2022

TOFAUTI ZA WENZA KATIKA KUFIKIRI NI MOJA YA CHANGAMOTO SUGU KATIKA MAHUSIANO

Maisha ya kimahusiano ya maelfu kama siyo mamilioni ya Wenza yamekuwa yakikumbwa na changamoto kubwa inayoambatana na kuwa na mabishano ya hapa na pale na kulaumiana wakati mwingine kwa sababu ndogo ndogo tu.

Na kwa hakika mabishano ya hapa na pale na kulaumiana ni bomu baya mno kwenye ustawi wa uhusiano wowote ule, na kiini kinachosababisha mabishano ya mara kwa mara na kulaumiana huko ni kwa kuwa wengi hatujui tofauti ya mwanaume na mwanamke kwenye kukabiliana na mambo.

Wanawake hua wanataka wanaume wafikiri kama wao na wanaume huwa wanataka wanawake kufikiri kama wanaume  kitu ambacho hakiwezekani  na hakitakuja kuwezekana  mpaka mwisho maisha Duniani.

Kimsingi ni kwamba asili ya akili ya mwanamke na mwanaume ni tofauti na fikra zao huwa tofauti hata kama wanashughulikia jambo moja.

Wadadisi wa mambo ya Saikolojia wanasema kwamba mwanamke anaweza kutazama Tv huku anatumia simu na akaweza kukumbuka vyote kwenye Tv na kwenye simu lakini mwanaume hawezi.

Mwanaume hawezi kufikiri vitu vingi kwa pamoja tofauti na mwanamke lakini wanawake hilo wengi hawajui hivyo wanaweza kueleza matatizo kibao wakidhani mwanaume anaweza kuelewa vyote kwa pamoja.

Inaelezwa kwamba Mwanaume akifikiria vitu zaidi ya kimoja kwa pamoja anachanganyikiwa haraka na kupoteza dira ya maamuzi sahihi.  Kwa kifupi wanaume wengi hawazielewi akili za wanawake na wanawake wengi hawazielewi akili za wanaume (hawaelewani) na hii ni changamoto sana.

Kwa mfano.
1. Mwanaume akiwa na stress huwa anataka kukaa kimya bila usumbufu aanze kufikiria matatizo yake mpaka apate ufumbuzi au Akishindwa kupata ufumbuzi huamua kukaa kimya analala, lakini mwanamke ni tofauti, akiwa na stress huwa anataka kuongea maumivu yake yote mpaka yaishe ndio stress zake ziondo, Kama akianza kulalamika tu utaona mwanaume anaanza kumpa ushauri, kumkosoa, kumpa ufumbuzi wa matatizo yake, kitendo hicho huzidisha maumivu na hasira kwa mwanamke na hali hiyo hufanya mwanamke azidi kulalamika sana.

Mwanamke akianza kulalamika kupita kiasi husababisha mwanaume kuchanganyikiwa na kuamua kujibu jeuri au kukaa kimya au kuondoka eneo la tukio..😂, na akiondoka tu hufanya mwanamke kupata hasira na kujiona kama anakosa upendo anaostahili...🤣 Nyieee  🙌

Kitendo cha mwanamke kuona anakosa upendo anaostahili humfanya apunguze kujituma ndani ya nyumba na kuacha kuheshimu juhudi za mwanaume(unaona kazi hiyo!). Mwanaume naye akiona juhudi zake hazipewi heshima hupata hasira na kulalamika sana na mwanamke akiona lawama zimezidi huzidi kuwa na hasira kwa kuona hakuna jema analofanya ndani ya nyumba yao!😄 na hapo migogoro huzidi kupita kiasi na malalamiko huongezeka kutoka kila upande.

2. Mwanamke: Anaacha vitu zig zagg anasambaza uchafu kila  mahali anashindwa japo kunisaidia   kupanga vitu     vizuri..?  haki nimechoka kusafisha nyumba kila akimaliza kula.

    Mwanaume: Yaani huyu mwanamke hana shukrani kabisa kila siku lazima atanilaumu kuwa nimekosea sehemu ..🤣

    Mwanamke: Umekaa tu kwenye Tv wakati nipo na nafanya kazi zote za nyumbani pekeangu nimechoka mimi sio mfanyakazi wake Mwanaume hajigusi asee jamaa hapana😄

Mwanaume: Anataka kila kitu kiwe safi hivi sasa kwanini asi-relax ?

Mwanamke: Yupo busy muda wote hajibu text zangu k,siwezi kumtegemea kwa chochote ni kama  hajali  tena hisia zangu ..

Mwanaume: Huyu mwanamke anakazi ya kukumbuka  makosa yangu tu na na hakumbuki wema hata mmoja jamani  kwamba sijawahi kumfanyia mazuri hata siku moja?🤔

Mivutano hasa kwenye mazungumzo yahusuyo pesa nayo mara nyingi huisha kwa kuibua maneno mengi.

Kutosaidiana kazi nyumbani poa huibua manunguniko kwa kushindwa kusomana akili na kutambuana.

Ubusy uliopitiliza kwa wanaume na baadhi ya wanawake pia, lakini yapo pia malalamiko ya kukosa muda wa pamoja, Malalamiko ya kutokukusikilizwa na kusikiliza, Hasira zilizo pitiliza, Kulinganisha maisha ya mwanzo wa uhusiano wenu na ya sasa na mengine mengi

Hivyo ni muhimu sana kujitahidi kujuana na kila mmoja kumfahamu mwenzie ili kupunguza hizi kero ndogo ndogo nyumbani

Haya mambo wanandoa au watu walio kwenye uhusiano huyachukulia poa sana na kuhisi ni kawaida ila hapa ndipo kifo cha uhusiano wenu kilipojificha.

Mwandishi: Hanifa Kafashe -Malikia wa Kiha


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages