LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 8, 2022

RAIS SAMIA ALIVYONOGESHA SHEREHE ZA KITAIFA YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, ILIYOFANYIKA JIJINI ZANZIBAR, LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Husein Ali Mwinyi baada ya kuhutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo Machi 8, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Maisara Zanzibar leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na  mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Mzee Abeid Amani Karume Bi Fatma Karume, baada ya kuhutubia katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Maisara Zanzibar leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiagana na Marais Wastaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume na Dk. Ali Mohamed Shein,baada ya kuhutubia katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Maisara Zanzibar leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokuwa akicheza pamoja na Kikundi cha ngoma za asili cha Bomu kutoka Unguja kabla ya kuhutubia Viongozi mbalimbali waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Maisara Zanzibar leo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Maisara Zanzibar leo tarehe 08 Machi, 2022.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages