Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (aliyevaa fulana nyeupe) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ifulifu.
Jimbo la Musoma Vijijini lenye KATA 21 lina jumla ya SEKONDARI 22 za Kata. Sekondari za Binafsi ni mbili (2).
Kata pekee isiyokuwa na Sekondari yake ni ile ya IFULIFU. Baadhi ya Kata zinazo Sekondari mbili na nyingine nazo zimeanza ujenzi wa sekondari ya pili ya Kata zao.
KATA YA IFULIFU
Kata hii ina Vijiji vitatu (3) ambavyo ni Kabegi, Kiemba na Nyasaungu.
Mradi wa Serikali yetu wa SEQUIP (Secondary Education Quality Improvement Programme) umetoa SHILINGI MILIONI 470 kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Kata ya Ifulifu.
Wanavijiji na Viongozi wa Kata hii na Jimbo lote kwa ujumla, wanamshukuru sana sana RAIS wetu, Mhe SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuona umuhimu wa kuchangia ujenzi wa Sekondari ya Kata hii ulioanza Juni 2017 na ulikuwa unasuasua kwa ajili ya ukosefu wa fedha za ujenzi.
UJENZI WA AWALI wa Sekondari ya Kata ya Ifulifu ulifanywa na Vijiji viwili vya Kabegi na Kiemba.
MICHANGO ya awali ya ujenzi wa Sekondari hii ilitolewa na WANAVIJIJI na MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo. Miundombinu iliyokuwa imejengwa ni BOMA la Vyumba vya Madarasa mawili (2) na Msingi wa Jengo la Utawala.
Kutokana na Jiographia ya Kata hii, Kijiji cha tatu cha Nyasaungu kilicho mbali na vijiji vingine, kimeamua kujenga Sekondari yake.
PROF MUHONGO AKAGUA UJENZI WA IFULIFU SEKONDARI
Jumanne, tarehe 8.3.2022, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ALIKAGUA ujenzi wa Ifulifu Sekondari unaoendelea Kijijini Kabegi.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇