LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 5, 2022

SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA NA KUWEKA MAZINGIRA BORA NA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA


Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaudi Kigahe akizungumza wakati wa  utoaji wa Taarifa  ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara  pamoja na Taasisi zake kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Februari 3, 2022  katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Mbunge wa Buchosa, Erick Shigongo akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Mbunge wa Njombe Mjini, Deo Mwanyika  akichangia hoja wakati wa kikao hicho.








Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaudi Kigahe (Mb.) amesema Serikali itaendelea kuboresha na kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji na wafanyabiara nchini ili kukuza uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya Taifa na kwa wananchi kwa ujumla.


Mhe. Kigahe ameyasema hayo  wakati wa utoaji wa Taarifa  ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara  pamoja na Taasisi zake kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Februari 3, 2022  katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Akitoa majumuisho ya maoni na mapendekezo ya wajumbe wa kamati hiyo, Mhe. Kigahe amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira bora na kuwalinda  wawekezaji na wafanyabiasha ili waweze kukua  na kushindana na masoko ya kikanda na kimataifa  pamoja na kuwawezesha kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyosaidia nchi kujitosheleza kwa bidhaa muhimu mbalimbali kama Sukari. 


Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Makiposa(Mb.) amesema Wizara inatakiwa kuendelea  kuboresha na kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji na wafanyabiashara, kupanua uwigo wa upatikanaji wa hiduma hadi vijijini pamoja na kusimamia uzalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini kwa kitumia malighafi za ndani ili kukuza uchumi wa nchi. 


Naye, Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Erick Shigongo (Mb) ameishauri Wizara kuanzisha mfuko wa ubunifu nchini (Tanzania Innovation Fund) kwa lengo la kulea, kuendeleza na kukuza vijana wabunifu wa bidhaa mbalimbali ambazo zinaweza kuanzisha viwanda vikubwa vya uzalishaji vitakavyoongeza pato la Taifa na ajira nchini.


Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali  yanayolenga kuboresha utekelezaji wa jitahada mbalimbali katika kuendeleza Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ikiwemo kuboresha mifuko ya kuwezesha Wajasiliamali, Kulinda wazalishaji wa ndani, kutafuta masoko ya uhakika ya mazao nje ya nchi, kutoa elimu kwa umma na kuongeza ubunifu katika kitumia malighafi zinazopatikana nchini katika kutengeneza bidhaa mbalimbali nchini.


Akitoa taarifa hiyo ya utekekezaji wa bajeti ya Wizara kwa wajumbe wa kamati hiyo,  Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Alfred Mapunda  alisema katika utekelezaji wa bajeti hiyo, Wizara imepata mafanikio mengi ikiwemo uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na biashara, uanzishaji wa kongani za viwanda, uboreshaji wa masoko ya mipakani, utoaji wa huduma kwa njia ya mtandao na  kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya nchi, kikanda na kimataifa.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages