BOTI KUBWA mbili za kuchukua abiria 80 zimeondoka Kisiwani Rukuba saa 10 alfajiri kupeleka WAWAKILISHI wao kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 45 ya CCM zinazofanyika Musoma Mjini.
Kisiwa cha Rukuba ni moja ya vijiji 3 vya Kata ya Etaro ya Jimbo la Musoma Vijijini.
WAKAZI wa Kisiwa cha Rukuba wanaendelea kutoa SHUKRANI nyingi sana kwa RAIS wao, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia SHILINGI MILIONI 250 kujenga Kituo cha Afya kisiwani humo.
UJENZI umeanza na WAKAZI wa Kisiwani humo wamechangia ifuatavyo:
(i) NGUVUKAZI:
*wanasomba mawe, kokoto na maji ya ujenzi. Vilevile, wanachimba misingi ya majengo yote.
(ii) SERIKALI YA KIJIJI/KISIWA
*Imetumia mapato yake kununua vifaa vya kutumiwa kwenye ujenzi - pump 2 za kuvutia maji kutoka Ziwani na mipira yake, mapipa ya kutunzia maji ya ujenzi.
FEDHA za UVIKO/IMF:
Fedha ziko kwenye Akaunti ya Zahanati yao na tayari zimeanza kutumika kununua:
*Saruji Mifuko 599
*Nondo 210
*Mbao 32 za 1×8
20 za 2×2
*Dawa ya kuua mchwa
TAARIFA hiyo hapo juu imetolewa na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji/Kisiwa, Ndugu Japhari Ibrahim Kabasa
PICHA zilizoambatanishwa hapa zinaonesha WAKAZI wa KISIWA cha RUKUBA wakisomba SARUJI iliyonunuliwa Musoma Mjini na kusafirishwa hadi Kisiwani humo.
PICHA moja inamuonyesha KIONGOZI (aliyekiti kwenye kiti) akihakiki SARUJI inayosombwa kutoka kwenye boti.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇