FEDHA za Ruzuku sh. mil. 250 zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika Kata ya MAKOJO Musoma Vijijini kwa ajiliya ujenzi wa Kituo cha Afya zimechangia kwa kiasi kikubwa kwa wananchi wa kata hiyo kuongeza kasi ya kushiriki ujenzi huo.
Wananchi wa Kata hiyo ya Makojo yenye Vijiji 3 (Chimati, Chitare na Makojo) wameamua kujitokeza kwa wingi katika ujenzi wa Kituo cha Afya ili kukikamilisha haraka iwezekanavyo.
WANAVIJIJI wanachangia NGUVUKAZI zao kwa kuchimba misingi ya majengo, kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi.
Kwa Mwaka huu wa Fedha, 2021/2022, Jimbo la Musoma Vijijini linajenga VITUO 2 vya AFYA:
VITUO vilivyokwishajengwa na vinavyotoa HUDUMA za AFYA ni:
*Murangi
*Mugango
*Bugwema
WANANCHI na VIONGOZI wa Kata ya Makojo wanatoa shukrani nyingi sana kwa SERIKALI yetu inayoongozwa kwa umahiri mkubwa na RAIS wetu, Mhe SAMIA SULUHU HASSAN.
VIONGOZI wa Vitongoji wanahamasisha ushiriki wa Vitongoji vyao kwenye utekelezaji wa Mradi huu.
DIWANI wa Viti Maalum, Mhe Tabu Maregesi Machumu anasimamia ujenzi huu kwa ufanisi na mafanikio makubwa - tunampongeza sana!
MABOMA 2 tayari yanakaribia kuezekwa:
*OPD
*MAABARA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇