LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 22, 2022

NAIBU WAZIRI SAGINI ALONGA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MARA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ally Salum Hapi katika moja ya ziara zake katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo iliyopo  Manispaa ya Musoma, mkoani Mara leo.


Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ally Salum Hapi akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini katika ofisi yake na kuahidi kutoa ushirikiano unaohitajika katika kila sekta na vyombo vya usalama vilivyomo katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenye Mkoa wake.


Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ally Salum Hapi akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumannne Sagini ukarabati wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara iliyopo Manispaa ya Musoma, leo Mkoani Mara.



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amekutana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Samwel Kuboye, pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM, Mara katika ziara yake Mkoani hapo leo, amewaomba washirikiane ili kudhibiti uhalifu uliopo mkoani Mara. 


Na Mwandishi wetu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne A. Sagini amefanya ziara mkoani Mara kwa kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara pamoja na kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama jimboni kwake Butiama.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ali Salum Hapi na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, Sagini amesema kuwa kwa  nafasi yake ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jukumu lake kubwa ni kuhakikisha usalama na amani ya nchi. Ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama kuendelea kushirikiana kudhibiti uhalifu unaojitokeza.

Naibu Waziri Sagini aliyasema hayo jana, 21 Januari 2022 alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Wilaya ya Musoma, mkoani Mara katika moja ya ziara yake.

“Moja ya changamoto ninayolenga kuidhibiti ni matukio ya uhalifu yanayojitokeza mara kwa mara Mkoani Mara na nchini kwa ujumla, hivyo navitaka vyombo vya usalama kuongeza nguvu zaidi kutokomeza matukio hayo. 

Aidha Naibu Waziri Sagini ameshangazwa na kauli za baadhi ya wananchi wanaosema uhalifu utarudi kwa kasi kwasababu ya mawaziri wapya wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Anasema IGP hajabadilishwa, Makamanda wa Polisi Nchi nzima ni wale wale, sasa uhalifu utaongezeka kivipi?

 “ Kuna maneno yanayosemwa kwamba uhalifu utarudi kwa kasi sasa hivi, naomba niwatoe hofu kwani IGP ni yule Yule, Makamanda wa Polisi ni wale wale, amani na usalama wa nchi utazidi kuimarika”

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mh, Ally Salum Hapi amefurahia kwa ujio wake na kuahidi kutoa ushirikiano unaohitajika katika kila sekta na vyombo vya usalama vilivyomo katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenye Mkoa wake.


Mwisho.




 


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages