Walioshuhudia wanasema idadi ya waliouwawa huenda ikawa juu zaidi na kufikia 200 kuliko ile iliyotajwa na serikali. Kulingana na ripoti za polisi baadhi ya majambazi waliovihangaisha vijiji hivyo pia waliuwawa.
Hadi sasa haijawa wazi iwapo washambuliaji ni wanachama wa kundi la wanamgambo la Boko Harram au ni magenge ya majambazi.
Wafugaji wa zamani waliounda makundi yao ya kijangili mara nyingi huwahangaisha wakaazi wa eneo hilo wakijaribu kuiba mifugo yao pamoja na ardhi zao licha ya maafisa wa usalama kuwepo katika maeneohayo.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇