LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 9, 2022

CCM YATANGAZA MCHAKATO WA MGOMBEA WAKE WA USPIKA, UCHUKUAJI FOMU KUANZA KESHO

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza mchakato wa kumpata Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Spika wa Bunge hilo Job Ndugai, ambapo kimesema mchakato huo unaaza kesho Jnauari 10, 2022.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, Zanzibar, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema Uchukuaji fomu kwa Wabunge w CCM kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo unaanza kesho, Januari 10, 2022 na mwisho wa kuchukua fomu na itakuwa Januari 15, 2022 ambayo ndiyo siku ya kurejesha fomu hizo.

Amesema Januari 17, 2022 Kitafanyika Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kujadili wagombea na kuishauri Kamati Kuu juu ya Wagombea ambao wamejitokeza kuomba kiti hicho cha Uspika kwa tiketi ya CCM.

Shaka amesema, Kitafanyika Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu  kitafanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 18 kwa ajili ya kufanya kazi ya kuchuja na kufanya uteuzi wa mwisho.

Amesema, kuanzia Januari 21 hadi Januari 30, Wabunge wa CCM watapiga kura kumpata Mbunge ambaye atakwenda kusimama Bungeni kwa ajili ya kuomba kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Nachukua fursa hii kuwataka Watanzania ambao wanakidhi vigezo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na Katiba ya CCM, wajitokeze kuomba nafasi hiyo ya Ubunge. CCM ipo salama, CCM ipo Imara Cchini ya Uongozi wa Mwenyekiti wetu Ndugu Samia Suluhu Hassan", amesema Shaka akihitimisha taarifa yake kwa Waandishi wa Habari.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Waandishi wa Habari , Katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar, leo.(Picha Na Fahadi Siraji - CCM)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages