Katika ujumbe aliouandika kupitia ukurasa wake wa twitter, Waziri Mkuu Boris Johnson alisema virusi vya corona vimeipiga vibaya nchi hiyo na idadi ya vifo vinavyorekodiwa vimefikia 150,000.
Hata hivyo Idadi ya wanaoambukizwa kila siku imepungua kutoka laki mbili wiki iliyopita hadi laki moja na nusu ndani ya saa 24.
Uingereza sasa imetoa masharti mapya ya kukabiliana na maambukizi hayo ikiwemo uvaaji wa barakoa kwa watoto wa shule wakiwa madarasani kwa wale watakaotaka huku kukusanyika kwa watu wengi kukipigwa marufuku. Urusi imebakia kuwa taifa la Ulaya lililo na idadi kubwa ya vifo vitokanavyo na virusi vya corona ambavyo hadi sasa vimefika 315,000.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇