Makongo, Dar es Salaam
Umoja Wanawake Tanzania (UWT), Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, umehimiza wanawake kujitokeza kwa kujisajili kidigitali uanachama ili kupata sifa za kuwa wanachama halali, kuwania nafasi za uongozi na kushiriki uchaguzi wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa UWT wa Wilaya ya Kinondoni, Anna Hangaya (Mama Makete),i alipokuwa akizungumza katika mafunzo ya utendaji kwa viongozi wa UWT Kata ya Makongo Juu, Dar es Salaam.
Mwenyekiti huyo amesema inasikitisha kuona katika usajili wa kidigitali unaofanywa na CCM, UWT imeshika nafasi ya tatu katika jumuiya za Chama, ambapo Jumuiya ya Wazazi inaongoza, ikifuatiwa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM).
“Haiwezekekani wanawake ambao ndiyo tegemeo la Chama tukashika nafasi ya tatu. Naomba wanawake wa UWT, jitokezeni kwa wingi kujisajili kidigitali ili taarifa zenu zitambulike. Usipo jisajili utakosa sifa ya kushiriki hata uchaguzi ndani ya Chama,”ameeleza Anna.
Mebainisha pia usajili huo ni muhimu katika kulinda matawi , mashina na kata kwani kama akidi hatatimia shina linaweza kuunganishwa na shina lingine, au tawi linaweza kuvunjwa ama kata ikaunganishwa na kata nyingine.
“CCM inasajili wanachama katika mfumo wa kigitali hivi sasa.Kadi za UWT zipo kwa viongozi. Nawasihi mno wanawake tujitokeze. Tufike katika ofisi zetu za Chama tujisajili. Uchaguzi unakuja tusije tukakosa sifa za kushiriki”, amehimiza Anna.
Pia amehimiza wanawake kujitokeza kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi wa ndani wa CCM kwani ni muda wa wanawake kushika dora.
“Jemedari wetu Samia (Rais Samia Suluhu Hassan), sasa tuko na Spika Tulia Akson mwanamke. Jitokezeni tuwaunge mkono. Mkituletea wagombea wazuri mimi nitakacho fanya ni kutenda haki tu.Ila na mimi nagombea ,”alimeeleza.
Alimpongeza Mwenyekiti wa UWT wa Kata ya Makongo Juu, Abiant Kivea, kwa kuandaa mafunzo hayo kwa watendaji wa UWT ngazi ya Kata na kwamba yanatija kubwa kwa maendelea ya Jumuiya.
Awali akizungumza,Mwenyekiti wa UWT wa Kata ya Makongo Juu, Abiant Kivea , alisema dhamira ni kuwakumbusha majukumu watendaji hao wa UWT katika kusimamia shughuli za Jumuiya na CCM.
Abiant amesisitiza wanachama wa umoja huo katika kata hiyo, kujitokeza kwa wingi kujisajili kidigitali ambapo usajili huo unafanyika nyumba hadi nyumba, mtaa kwa mtaa na katika ofisi zote za Chama.
“Wale vijana wote waliofikisha umri wa miaka 18 waitwe kwenye jumuiya wapewe kadi na wasajiliwe. Huku CCM ni kuzuri. Tumebakiza siku chache za usajili kidigitali. Kadiza CCM zinapatikana kwa kila Mjumbe wa Shina na kadi za UWT zinapatikana katika matawi yote” ameeleza Abiant.
Katibu wa UWT wa Kata ya Makongo, Deodata Komba, aliwataka wakina mama kuwapa ushirikiano wa kutosha vijana wanao pita mitaani kwaajili ya usajili kwani Makongo ni Kata ya ushindi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), wa Wilaya ya Kinondoni, Anna Hangaya (Mama Makete) akizungumza wakati wa mafunzo ya uongozi kwa Watendaji wa UWT Kata ya Makongo, Dar es Salaa. Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wa Kata hiyo Abiant Kivea na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata Miraji Said Rangi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇