LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 23, 2022

MAZISHI YA MWANAMUZIKI DEFAO WA CONGO-DRC ALIYEFARIKI MWAKA JANA, YAFANYIKA JANA

BBC, Gongo-DRC
Aliyekuwa Mwanamuziki nguli wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Congo-DRC) François Lulendo Matumona, maarufu General Defao ambaye alifariki Disemba 27, mwaka jana katika Hospitali Laquintinie mjini Douala, Cameroon, amezikwa katika mazishi ya Kitaifa jana, Jumamosi, Januari 22, 2022, mjini Kinshansa.

Inlelezwa kuwa Defao amechelewa kuzikwa kufuatia mvutano uliotokea kati ya Chama cha Wanamuziki Nchini DRC kikiongozwa na Mkongwe Adios Alemba na Ndugu Shaka Kongo ambae hutetea haki za Wanamuziki, Kila mmoja akitaka yeye ndie awe msimamizi wa shughuli za mazishi.

Familia ya Marehemu kwa upande wao waliitaka Serekali ya Congo iharakishe mambo ili mpendwa wao Defao awekwe kwenye nyumba yake ya milele.

Wakati wote Mdogo wake Defao, Chirac Lulendo alikuwa tayari yupo Douala Cameroon akisubiri maelekezo ya Serikali maana hadhi aliyokuwa nayo Mwanamuziki huyo siyo ya Kifamilia, bali ya Kitaifa na Kimataifa.

Kwa upande mwingine, Wizara ya Utamaduni ilikuwa imeshatoa pesa nakuzituma kwenye Ubalozi wa Congo nchini Cameroon kwa ajili ya maandalizi ya kuurudisha Congo mwili wa Marehemu Defao.

Kamati iliyoundwa kwa ajili ya kutoa maamuzi kamili ya mazishi, lini mwili wa Marehemu Defao ungefikishwa Kinshansa, Wangapi wangesafiri kurejea na mwili na ni sehemu gani atazikwa.

Taarifa kutoka kwa jamaa zake wanasema Mwanamuziki huyo hakuacha mtoto lakini ameacha vito vya dhahabu vya thamani ya Dola 260 za Kimarekani ambavyo ni mikufu ya dhahabu aliyokuwakuwa akivalia shingoni.

Wanamuziki wenzake na mashabiki wake waliohudhuri mazishi hayo wakiwa wamevalia mavazi za bei ghali wakidai pia Defao alikuwa mmoja wao, na wanafanya maonesho ya mavazi.

Defao aliyezaliwa Kinshasa Disemba 31, 1958, alianza kuimba muziki mwaka wa 1978 kama sehemu ya Orchester Suka Movema, pia alicheza kwa muda mfupi na Fogo Stars na Somo West kabla ya kujiunga na Grand Zaiko Wawa na baadaye kuwa sehemu muhimu ya Choc Stars.

Mwimbaji huyo wa wimbo wa Sala Noki atakumbukwa sana kwa sauti yake nzuri na miondoko ya dansi ya ambayo ilivutia wengi.

Ilikuwa katika kipindi hiki ambapo Defao aliboresha ustadi wake wa uimbaji na uandishi wa nyimbo, akifanya kazi na watu wa nyumbani wakati huo kama Ben Nyamabo na Bozi Boziana.

Katika azma yake ya kujitengenezea nafasi nzuri, Defao aliachana na Choc Stars kuelekea mwisho wa 1990 na kuunda Big Stars na Djo Poster.

Hata hivyo, mambo hayakwenda kulingana na mipango yake na alilazimika kutafuta wanamuziki wapya baada ya Djo kuondoka.

Katikati ya miaka ya 90, Defao alikuwa tayari akitishia kufuta majina maarufu kama Koffi Olomide na Bozi Boziana kutoka ulingo wa muziki lakini hakufaulu kupata umaarufu nje ya nchi.
Jeneza lenye mwili wa Defao likiwa limewekwa katika eneo la kuagia kabla ya mazishi.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages