Jan 12, 2022

MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO AHUDHURIA MKUTANO WA SADC NCHINI MALAWI, LEO AONDOKA KUREJEA NYUMBANI BAADA YA KIKAO HICHO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akishiriki katika mkutano wa Dharura wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu wa Mutharika Lilongwe Nchini Malawi. Januari 12, 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiungana na viongozi wengine katika kuwakumbuka askari na raia waliopoteza Maisha katika mapigano yanayoendelea nchini Msumbiji wakati wa mkutano wa Dharura wa wakuu wa Nchi na Serikali Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu wa Mutharika Lilongwe Nchini Malawi. Januari 12, 2022.

Wakuu wa Nchi na Serikali Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa Mkutano wa Dharura wa SADC uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu wa Mutharika Lilongwe Nchini Malawi. Januari 12, 2022. Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango (Watatu kushoto, Mstari wa nyuma) akiwa miongoni mwa viongozi hao.


Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akiagana na Viongozi wa Malawi alipokuwa akiondoka kurejea nchini leo baada ya mkutano huo wa SADC. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages