LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 20, 2022

MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO AFIWA NA KAKA YAKE

Na CCM Blog, Dar es Salaam

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amefiwa na kaka yake Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Gerald Mpango. 


Taarifa zimesema, Askofu Gerald Mpango amefariki jana, Januari 19, 2022 Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. 


Enzi za uhai wake Askofu Gerald Mpango alihudumu katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Magharibi ya Tanganyika ( Diocese of Western Tanganyika)

 

Taarifa zimesema, mazishi ya Askofu Mstaafu Gerald Mpango yanatarijiwa kufanyika siku ya Jumamosi,  Januari 22, 2022 wilayani Kasulu Mkoani Kigoma. 


Kwa mujibu wa taarifa hizo, mazishi hayo yatatanguliwa na ibada ya kuaga mwili wa marehemu itakayofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano lililopo Posta Jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa, Januari 21 2022.


Baada ya mwili kuagwa jijinj Dar es Salaam utasafirishwa kwenda mkoani Kigoma ambako pia itafanyika Ibada ya kuaga mwili katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea Kasulu Kigoma.

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akiwa katika na  Askofu Mstaafu Gerald Mpango, Desemba 16, 2021 wakati Makamu wa Rais alipofanya ziara mkoani Kigoma👇

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages