LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 20, 2022

KAMATI KUU YA CCM YAMPITISHA DK. TULIA ACKSON KUGOMBEA USPIKA WA BUNGE

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson

 

Na CCM Blog, Dodoma
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, imepitisha jina la Naibu Spika wa Bunge Dt.Tulia Ackson kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, amesema Kamati Kuu katika Kikao chake kilichofanyika leo, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, kwa taratibu na mujibu wa Katiba ya CCM pamoja na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo majina ya waliowania nafasi ya Spika wa Bunge kimefikia uamuzi wa kumteua Dk. Tulia kuwania nafasi hiyo.

“Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ilipitia na kuchambua majina ya waliochukua fomu za kuwania nafasi ya uspika na kisha baada ya kujiridhisha imemteua Naibu Spika Tulia Akson kuwania nafasi hiyo na sasa hatua inayofuata ni kikao cha Wabunge wanaotokana na CCM) kumpigia kura katika kikao chao kitakachofanyika Januari 30, mwaka huu.

Shaka amesema, Kamati Kuu imempongeza Rais Samia, katika utendaji wake kuhakikisha Wanafunzi wote nchini wameingia Kidato cha kwanza kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa madarasa huku kikimpongeza pia Rais wa Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi kutokana na utendaji wake kwa kusimamia uchumi wa buluu.

“Chama kimefuatilia kwa ukaribu sana utendaji wa Serikali na kimejiridhisha na kazi nzuri zinazofanywa na Marais wa pande zote mbili Bara na Zanzibar", amesema Shaka.

Uchukuaji fomu ambao ulikuja kufuatia aliyekuwa Spika wa Bunge Job Ndugai kujiuzulu mnamo Januari 6, 2022, na ulinza Januari 10, 2022 hadi Januari 15, 2022, ambapo waliochukua fomu walifikia 71 na waliorudisha ni 70.na mmoja ndiye hakurudisha.
 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Kikao cha kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taiva ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika leo jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages