Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti wa Kike Tanzania (Tanzania Girl Guides Association ,TGGA), Mary Richard, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya mabadiliko ya Tabianchi yaliyoshirikisha wakufunzi kutoka nchi za Tanzania, Benin na Lesotho. Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Januari 22, 2022 katika Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini Dar es Salaam.
Meneja wa Programu ya Mabadiliko ya Tabianchi wa TGGA, David Mbumila akielezea muhtasari wa mafunzo hayo.
Sehemu ya wakufunzi kutoka mikoa 12 nchini na wengine kutoka nchi za Benin na Lesotho wakiendelea na mafunzo hayo.
Baadhi ya wakufunzi kutoka mataifa mbalimbali wakitambulishwa .
Viongozi vijana wa TGGA wakitambulishwa
Baadhi ya wakufunzi wa kujitolea kutoka Uingereza, Ufaransa na Hispania kutoka Chama cha Skauti wa Kike Duniani (WAGGGS).
Baadhi ya wakufunzi wakiwa katika mafunzo hayo.
Wakufunzi wakibadilishana mawazo kuhusu mabadiliko ya Tabianchi ikiwa ni sehemu ya mafunzo hayo
Mkufunzi Alice Kestell akimsikiliza mtoto Mytham Ameir mwanachama wa TGGA ngazi ya watoto ya Tanzanite wakati wa mafunzo hayo. Mtoto huyo ameambatana na mama yake mzazi Rose Goima ambaye ni mmoja wa wakufunzi waliohudhuria mafunzo hayo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Kamishna Mkuu, Mary Richard na Meneja wa Programu ya mafunzo hayo, David wakielezea umuhimu wa mafunzo hayo....
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇