LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 20, 2022

ALIYECHAPWA BAKORA NA NDUGAI, AMPONGEZA DKT TULIA KUPITISHWA NA CCM KUWA MGOMBEA USPIKA


 Dkt Simon Ngatunga ambaye alikuwa miongoni mwa wanaCCM 69 waliochukua na kurejesha fomu za kuomba kuwania kiti cha uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameipongeza Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, iliyooongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson kuwa mgombea wa kiti hicho.

Ngatunga ambaye alichapwa kiboko na Spika aliyejiuzulu, Job Ndugai alipokuwa akiwania naye katika kura za maoni za kuomba kuwania ubunge katika jimbo la Kongwa mwaka 2015, ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma.


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Dkt Ngatunga akitoa pongezi hizo.....

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages