Diwani wa Kata ya Msalato, jijini Dodoma, Nsubi Bukuku akifungua semina ya Bodi ya Nyama Tanzania na wadau wa nyama choma na wauza nyama mbichi katika mnada wa Msalato, kwa lengo la kuwaelimisha jinsi ya kuiandaa nyama kwa usalama hadi kumfikia mlaji.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma.
TAMASHA la Nyama Choma linatarajiwa kufanyika katika Mnada maarufu wa Msalato, jijini Dodoma Jumamosi Desemba 11, 2021.
Tamasha hilo linaloratibiwa na Diwani wa Kata ya Msalato, Nsubi Bukuku kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi wa kata hiyo, pamoja wachoma nyama wa eneo hilo, litaendeshwa kwa mtindo wa kuwashindanisha na watakaoshinda watazawadiwa yawadi kem kem.
Ili kufanikisha tamasha hilo, Bodi ya Nyama Tanzania imeamua kuendesha mafunzo kwa wadau wa soko hilo jinsi ya kuandaa nyama kutoka machinjioni, kusafirisha, kuhifadhi na usafi wakati wa kuchoma na hatimaye kumuuzia mteja iliyo safi na salama. Mafunzo hayo zameendeshwa na Daktari wa Mifugo wa Bodi ya Nzama Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Olais Ngilisho.
Aidha, Bukuku amesema kuwa Tamasha hilo ambalo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, litahanikizwa na masuala ya muziki kutoka kwa wasanii, uonjaji wa mvinyo wa zabibu ya Dodoma lakini pia kila kona ya mnada huo kutawekwa Screen kubwa na ndogo kuwawezesha wapenzi wa soka kushuhudia pambano la watani wa jadi Yanga na Simba.
Daktari wa Mifugo wa Bodiya Nyama Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Olais Ngilisho. akiendesha mafunzo kwa wadau hao wa nyama choma na wauza nyama mbichi Msalato.
Mwenyekiti wa Nyama Choma Msalato, Haji Maulid akisistiza wadau hao kuzingatia mafunzo hayo yaliyotolewa na Bodi ya Nyama.
Afisa Afya Kata ya Msalato, Henry Mfugwa akisisitiya masuala ya afya kwa kuweka mazingira mazuri eneo la kuchomea nyama na unadhifu.
Baadhi ya wadau wakisikiliza kwa makini wakati wa semina hiyo ya Mchoma nyama,
Kutona Akida akiuliza swali wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti Msaidizi Wachinjaji, Aloyce Toiba akichangia mada.
Afisa Mifugo Kata ya Msalato, Dativa Kimolo akichangia mada wakati wasemina hiyo.
Mwenyekiti wa Wachinjaji Msalato, Abdul Ismaily akiwasisitiza wadau kukubali na kuyatekeleza yote waliyofundishwa na Bodi ili biashara yao iende vizuri.
Eneo la Mnada wa Msalato linavyoonekana siku za kawaida
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video, ujue yaliyojiri katika semina hiyo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇