Na Is-Haka Omar, Zanzibar
Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimetoa azimio la kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa maamuzi yake ya kuwarejeshea fedha zao wananchi waliokuwa wanaidai Kampuni ya Masterlife.
Pia kikao hicho kimempongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kutimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani, na kuridhishwa na uongozi wake wenye mafanikio makubwa yakiwemo kudumisha hali ya amani, utulivu na mshikamano kwa wananchi wote.
Kikao hicho cha siku moja kimefanyika leo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui kikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, ambaye pia ni Rais mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimepokea na kujadili taarifa mbalimbali za kiutendaji kutoka katika idara za CCM Zanzibar na pia kumepokea na kujadili taarifa ya ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk. Mwinyi aliyoifanya katika mikoa sita ya CCM Kichama.
Kikao hicho ni cha kawaida kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977, Toleo jipya la mwaka 2017, Ibara ya 108 (2), inayofafanua kwamba Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, itafanya mikutano yake ya kawaida mara moja kila miezi mitatu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kilichofanyia Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, mjini Zanzibar, leo. Katikati ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi.Wajumbe wakiwa wamesimama wakati Dk. Shein akiingia ukumbini kuongoza kikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein baada ya kuigia ukumbini. katikati ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi.Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Mabodi alipokuwa akifungua kikao hicho.
Kikao hicho kikiendelea.
©2021 CCM Blog/Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇