Aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Ngorongoro jijini Arusha Emmanuel Lekishon Shangai, ametangazwa mshindi kwa kuibuka mshindi katika Uchaguzi uliofanyika jana, Jumamosi, Disemba 11, 2021.
Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo, katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Msimamizi wa Uchaguzi huo Dk. Jumaa Mhina, alisema Shangai ameibuka na ushindi kwa kupata kura 62,017 Kati ya kura halali 62,461 akifuatiwa na mgombea wa ACT Wazalendo Johnson Gagu, aliyepata kura 170 kati ya kura 62,528 zilizopigwa.
Mgombea mwingine katika uchaguzi huo Saimin Paul Ngilisho wa Demokrasia Makini alipata kura 105 na Mohamed Kitundu wa ADC alipata kura 63 huku Mwinyi Hamisi wa ADA TADEA akipata kura 30, Mary Moses Daud wa UPDP akipata kura 20 na Wagombea Juma Feruziyson wa NRA na Amina Amir Mcheka wa NLD wakipata kura 16 kila mmoja.
Katika matokeo hayo ya Uchaguzi huo ambao umefanyika baada ya aliyekua Mbunge wa Jimbo hilo, William Ole Nasha kufariki dunia, Mwita Makuru wa UDP aliyepata kura 10, Saimon Johnson wa SAU kura 9 na Frida Marko Nko wa UMD kura 5.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngorongoro, Dk. Jumaa Mhina (Kulia) akikabidhi cheti cha ushindi wa Kiti cha Ubunge kwa Mbunge Mteule wa Jimbo la Ngorongoro, Emmanuel Lekishon Shangai baada ya kuibuka mshindi kwa kupata kura 62,017 Kati ya kura 62,528 zilizopigwa katika Uchaguzi Mdogo uliofanyika jana, Desemba 11,2021.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇