LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 1, 2021

BUNGE SPORTS CLUB YAAHIDI MAKUBWA MICHEZO YA MABUNGE AFRIKA MASHARIKI



Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba akimkabidhi Kaimu Katibu wa Bunge, Mohamed Mwanga sare za michezo na vifaa vingine kwa ajili ya Timu ya michezo za Bunge zitakazoshiriki mashindano ya mabunge Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza Desemba 4 jijini Arusha. Hafla hiyo imefanyika Ukumbi wa Habari bungeni Dodoma Novemba 30,2021.

Klabu ya Michezo ya Bunge (Bunge Sports Club), imeahidi ushindi mkubwa katika mashindano ya michezo mbalimbali yatakayoshirikisha mabunge ya nchi ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza kurindima Desemba 4, 2021 jijini Arusha. Akizungumza wakati wa hafla ya Kampuni ya SportPesa kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo kwa klabu hiyo, Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Abbas Tarimba amejinasibu mbele ya vyombo vya habari kuwa wamejiandaa kwenda kucheza vizuri na kutwaa ushindi wa jumla. SportPesa wadhamini wa klabu hiyo, imekabidhi vifaa vyenye thamani ya zaidi sh mil. 20.
Tarimba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, akikabidhi mipira.


Meneja wa Bunge Sports Club, Seif Gulamali akionesha moja ya sare za michezo walizokabidhiwa na SpoetPesa.


Mbunge wa Mchinga, Mama Salma Kikwete akitoa neno la shukrani kwa SportPesa kuidhamini Klabu ya Michezo ya Bunge.



Wabunge wanamichezo wakimwimbia Mama Salma Kikwete wimbo wasiku ya  kuzaliwa kwake alizoitangaza baada ya kutoa neno la shukrani.


 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia katika clip hii ya video ujue yaliyojiri katika hafla hiyo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages