Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma Novemba 30,2021 kuelezea tulikotoka, tulipo na twendako pamoja na changamoto na mafanikio kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Waziri Ummy pamoja na mambo mengine ameelezea pia azma ya Serikali kuboresha usafiri wa umma kwa kuanzisha Wakala wa Usafiri wa Haraka katika majiji mengine nchini ambayo ni Arusha, Tanga, Mwanza na Mbeya.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini wakati Waziri Ummy, akielezea changamoto na mafanikio ya wizara hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akizungumza wakati wa kuhitimisha mikutano ya mawaziri kuelezea changamoto na mafanikio ya wizara zao ndani ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Mikutano hiyo ilianza Novemba 2, 2021.
Waziri Ummy (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo, Gerson Msigwa wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Dkt Grace Magembe walipokuwa wakijadiliana jambo baada ya mkutano kumalizika.
Waziri Ummy akiondoka baada ya mkutano kumalizika.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Waziri Ummy pamoja na mambo mengine akielezea mipango hiyo ya kuanzisha usafiri wa haraka katika majiji nchini....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇