Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt Mashimba Ndaki leo Novemba 25, 2021, amezungumza katika mkutano na vyombo vya habari jijini Dodoma, kuelezea tulikotoka, tulipo na tunakoelekea zikiwemo changamoto na mafanikio ya sekta hiyo kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Pamoja na kuelezea mambo mbalimbali kuhusu hatua ilizopiga sekta hiyo, amesema kuwa kwa kawaida kila Mtanzania anatakiwa kila mwaka kula nyama zaidi ya kilo 50 lakini anakula kilo 15 tu, na kwa upande wa maziwa anatakiwa kunywa zaidi ya lita 200, lakini anakunywa wastani wa kijiko kimoja....
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo ambapo baadhi hupata kuuliza maswali.Waziri Ndaki akijadiliana jambo na Afisa Habari wa Idara ya Habari-MAELEZO, Immaculate Makilika baada ya kumalizika kwa mkutano huo ulioongozwa na afisa huyo.
Waziri Ndaki akiwa na viongozi wengine wa wizara hiyo.
Waziri Ndaki akiondoka kwa furaha baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Waziri Ndaki akielezea umuhimu wa watanzania kuongeza kiwango cha kula nyama na unywaji maziwa kwa mwaka...
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇