NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara,akikagua ujenzi wa nyumba 20 katika eneo la Kisasa zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) Jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara,akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa mradi wa nyumba 20 katika eneo la Kisasa zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) Jijini Dodoma.
Muonekano wa Mradi wa nyumba 20 za viongozi zinazojengwa na Wakala wa Majengo zilizopo eneo la Kisasa Dodoma.
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara,akikagua ujenzi wa mradi wa nyumba 150 zilizopo Nzuguni zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) Jijini Dodoma.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa mradi wa nyumba 150 zilizopo Nzuguni zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) Jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara akishiriki katika kuchanganya mchango pamoja na ujenzi katika mradi wa nyumba 150 zilizopo Nzuguni zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) mara baada ya kufanya ziara ya kukagua mradi huo Jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua nyumba 20 katika eneo la Kisasa na 150 zilizopo Nzuguni zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) Jijini Dodoma.
Meneja wa Wakala wa Majengo Mkoa wa Dodoma,Victor Balthazar,akimshukuru Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara, (hayupo pichani) mara baada ya kukagua nyumba 20 katika eneo la Kisasa na 150 zilizopo Nzuguni zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) Jijini Dodoma.
Mradi wa nyumba 20 za viongozi, Mkadiriji Majenzi Goddy Mduda,akielezea ujenzi wa nyumba za Kisasa ulipofikia mara baada ya Naibu Waziri ,Mwita Waitara kukagua nyumba 20 katika eneo la Kisasa zinazojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) Jijini Dodoma.
…………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara ameutaka Wakala wa Majengo (TBA) kuboresha kitengo cha ufuatiliaji ili kujua nyumba ambazo zimekuwa zikipangishwa na kisha wahusika kuwapangisha watu wengine.
Akizungumza Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua nyumba 20 katika eneo la Kisasa na 150 zilizopo Nzuguni ambazo zinajengwa na Wakala huo kwa ajili ya watumishi wa umma ,Waitara Naibu amesema kuwa TBA wanawajibu wa kuboresha kitengo cha ufuatiliaji.
“Ule mpango mtu anapewa nyumba anakaa kisha onaondoka anapewa mtu mwingine bila makubaliano kama mkataba aliingia na watu wa TBA akitaka kuondoka ni lazima ukague nyumba wakati anaingia ilikuwaje na wakati anatoa imekuwaje.
“Nyumba zetu hizi ni nzuri lazima kuwe na kitengo cha kufuatilia kuona matengenezo yakoje,hili mtoe uzito.Lazima mboreshe kitengo cha ufuatiliaji mfano Dodoma mahitaji ni makubwa lakini wanataka pia nyumba iboreshwe,”amesema.
Aidha,Waitara ameipongeza TBA kwa kujenga nyumba bora na zenye kiwango kinachokubalika ambapo amesema kuwa ujenzi wa nyumba hizo unatarajiwa kukamilika mwakani mwezi wa tisa.
“Tunatarajia Rais atakuwa anafuatilia,bahati nzuri mnajenga nyumba na mitambo ya kokoto na matofali ipo hapahapa hakutakuwa na kisingizio.Nimefurahi mnafanya kazi na mradi utaisha mwakani mwezi wa tisa na viongozi wanatarajia kuzitumia nyumba hizi,”amesema
Kuhusiana na kwamba nyumba hizo kodi kuwa kubwa,Naibu Waziri Waitara amesema nyumba hizo ni za watumishi na zimejengwa na Serikali hivyo gharama zake zitakuwa ndogo.
“Nyumba hizi ni za watumishi na zimejngwa na Serikali ili kumpunguzia maisha mtumishi tukipangisha watumishi wakatosha tutapangisha watu wengine.,”amesema.
Vilevile,Waitara amemshukuru Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi Mkoani Dodoma.
“Kwanza nimshukuru sana Rais (Samia Suluhu Hassan) kwa kutoa fedha ametoa fedha nyingi kwa mfano pale nyumba 20 makisio ni shilingi bilioni 5 na ameishatoa fedha yote kwahiyo watu wa TBA kazi kwao tunatarajia nyumba zikamilike kwa wakati
“Eneo hili mnaloliona ni ekari 680 ni eneo kubwa tunakusudia kujenga nyumba za kawaida hizi zaidi ya 3000 katika eneo hili na zitakuwa nyumba za ghorofa.Kwa hiyo huu ni mradi mkubwa ambao tumeanza kama sehemu ya mfano tunatarajiwa watu wa TBA wakifanya vizuri zaidi Mheshimiwa Rais ataendelea kutoa hela,”amesema.
Kwa upande wake,Meneja wa Wakala wa Majengo Mkoa wa Dodoma,Victor Balthazar amemshukuru Naibu Waziri kwa kutembelea mradi huo huku akiahidi watatekeleza kwa wakati mradi huo.
“Nataka nichukue nafasi hii kukushukuru kwa kutembelea mradi wetu wa Kisasa na Nzuguni uliyoasema tutayazingatia na nikuahidi tuyafanyia kazi,Tutatekeleza kazi hii ndani ya muda ambao tumejiwekea na kujipangia lakini iwapo itatatokea changamoto tutatoa taarifa mapema ili tuweze kujua tutaitekelezaje,”amesema.
Vivile,ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha kwa ajili ya mradi huo ambapo amedai kwa Mkoa wa Dodoma mahitaji ya nyumba kwa watumishi wa umma ni makubwa.
“Kama ulivyoeleza Mkoa wa Dodoma uhitaji wa nyumba ni mkubwa sana watumishi wengi hawana nyumba tunaishukuru Serikali kwa kuweza kutupatia fedha hizo tunaamini hatutamwangusha tutaitekeleza kazi hii kwa uadilifu,”amesema.
Amesema changamoto wanayokutana nayo kwa sasa ni kutokea kwa viashiria vya kuadimika kwa Saruji huku akidai suala la mchanga na kokoto wamelitatua.
“Tunajaribu tunakusanya mchanga mwingi na kokoto hata mvua itakapokuja tusipate shida kwani msimu wa mvua Dodoma huwa kunakuwa na shida jinsi ya kupata mchanga,”amesema.
Naye Mradi wa nyumba 20 za viongozi, Mkadiriji Majenzi Goddy Mduda amesema kuwa kati ya nyumba hizo zilizojengwa ni 19 Sawa na asilimia 50 ya kazi hivyo wapo kwenye umaliziaji.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇