JIMBO la Musoma Vij ijini kwa kutumia MICHANGO ya WANANCHI, MBUNGE wa JIMBO, MADIWANI na SERIKALI KUU (i.e. TAMISEMI) inajenga SHULE SHIKIZI 12 (kumi na mbili).
Kati ya hizo 12, Shule Shikizi tatu (Busambara, Kaguru na Mwikoko) zimepata FEDHA za UVIKO 19 (IMF) kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa.
Shule Shikizi Mwikoko, iko kwenye Kitongoji cha Mwikoko, Kijijini Chitare, Kata ya Makojo.
Sikiliza "CLIP" iliyoambatanishwa hapa - Wanakijiji wakiwemo Wanafunzi wanaongelea ujenzi wa Shule Shikizi yao ya Mwikoko.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇