LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 3, 2021

MBUNGE MAHAWANGA AZINDUA VIKUNDI VINANE VYA WANAWAKE KATA YA GONGOLAMBOTO, JIMBO LA UKONGA

Na Mwandishi Maalum, Ukonga

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Mahawanga Janeth amezindua vikundi vinane vya wanawake katika Kata ya Gongolamboto jimbo la Ukonga, kwenye shughuli maalum  iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Ukonga (Ukonga Women's Association) akiwa ameongozana na Diwani wa Kata ya Gongolamboto na  Madiwani wa Viti Maalum kutoka Jimbo ya Ukonga.


Mh. Mahawanga amefurahishwa na umoja wa Wanawake wa Ukonga kwa kuandaa shughuli hiyo ambayo pia iliwajumuisha Wanawake kutoka maeneo mbalimbali nje ya Jimbo la Ukonga kwa ajili ya kupata elimu ya Ujasiriamali, Fedha, Fursa, Matumizi ya Teknolojia ya Kimtandao na kujiunga na vikundi rasmi ambavyo dhumuni lake ni kuhakikisha wanamkomboa Mwanamke kiuchumi.


Mh. Mahawanga alitoa wito kwa vikundi mbalimbali ambavyo ni vikongwe na vimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhakikisha vinasaidia vikundi vipya na vile vichanga kwa kuwa nao karibu hasa kuwafundisha ili nao waweze kufikia lengo la kuwa na mitaji na biashara kubwa ambayo itawasaidia kwenye kukopeshana na kutoa mitaji kwa wanawake nje ya ile 4% tunayotengewa Wanawake kutoka kwenye Halmashauri zetu ili kuhakikisha lengo la kumkwamua Mwanamke wa Dar kiuchumi linafanikiwa.


Aidha  amesisitiza wanachama kupitia vikundi vyao kushirikiana pamoja sambamba na kudumisha Upendo, Umoja na Mshikamano pasipo kubaguana kulingana na kipato cha mtu mmoja mmoja ili kuhakikisha wanatimiza ndoto kubwa waliyonayo ya kusaidiana na kuinuana  sambamba na kukifikisha kikundi kwenye hatua nzuri ya kutengeneza ajira miongoni mwao.


Na mwisho alitoa wito kwa Wanawake wote wenye sifa kujitokeza  kugombea nafasi mbalimbali ndani ya Chama na kwenye Jumuia zake bila woga ili kuhakikisha tunakuwa mstari wa mbele katika kumsaidia Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kutimiza ndogo yake ya kuona Wanawake wa Tanzania wanakomboka kichumi. Lakini pia kuwa mstari wa mbele kupaza sauti kutetea mambo yote yanayomkandamiza Mwanamke na Mtoto wa Kitanzania,  kusimamia malezi bora kwa Vijana wetu ambao tunawaandaa kuwa Viongozi wazalendo wajao.

#TishaMama.

#ItazameDarKiutofau

#KaziIendelee.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages