LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 29, 2021

MBUNGE MAHAWANGA ASISITIZA KUENDELEA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KATIKA KUHAKIKISHA VIKUNDI VYOTE VYA WANAWAKE DAR VINASAJILIWA

Na CCM Blog Dar es Salaam
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Janeth Mahawanga amesisitiza juu ya msimamo wake wa kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha vikundi vyote vya Wanawake ndani ya mkoa huo vinasajiliwa.

Ameongeza kuwa, mbali na kuhakikisha vikundi vyote vya Wanawake vinasajiliwa pia azma yake ni kuhakikisha vikundi hivyo vinapata mikopo ya Halmashauri na wadau mbalimbali wa maendeleo, ili hadi kufikia 2025 Wanawake ndani ya mkoa wa Dar es Salaam wawe wameweza kujikwamua kiuchumi na kuzitumia fursa zilizopo ndani ya mkoa huo.

Mbunge Mahawanga amesema hayo juzi, wakati akifunga Semina ya vikundi vichanga vya Wanawake, iliyoendeshwa na Kikundi cha Women of Hope Alive, kwa ufadhili wa Uholanzi hapa nchini na kufanyika katika ukumbi wa Global hoel, jengo la Mkapa Tower jijini Dar es Salaam.

Akiwafunda wanavikundi waliohudhuria Semina hiyo, Mbunge Mahawanga alisisitiza wanawake kuendelea kuwa na Umoja na mshikamano katika vikundi vyao ili kuweza kufikia lengo kuu la kujikwamu kiuchumi, lakini sambamba na kufungua fursa mpya kwa wanawake wengine kuona umuhimu wa kujiunga na vikundi rasmi.

Aidha Mbunge Mahawanga alieleza kufurahishwa kwake sana kuona Wanawake mbalimbali wamejitokeza katika semina hiyo ya siku mbili  ambayo ilihudhuriwa na  wawakilishi kutoka vikundi 40 ambavyo kati yake 20 ni vichanga na 20 ni vipya kabisa.

"Nina imani kupitia wawakikishi hawa kupata semina hii ya siku mbili itasaidia sana kwenda kufikisha elimu hii kwenye vikundi vyao, ili kuongeza uelewa mpana wa umuhimu wa kusajili vikundi rasmi kwani mada zilizotolewa na wataalamu katika mafunzo hayo ni pamoja na Namna ya kuzitambua fursa mbalimbali.

Hali kadhalika Uendeshaji wa vikundi, Utunzaji wa kumbukumbu, Usimamizi wa fedha, Utatuzi na usuluhishi wa migogoro ndani ya vikundi, Usajili wa vikundi, Uendeshaji wa vikundi kwa mujibu wa sheria na upatikanaji wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo", akasema Mbunge janeth Mahawanga.

Alisema vile vile amefarijika kwamba washiriki wa Semina hiyo wamefundishwa kuhusu njia za kupambana na Ukatili wa kijinsia kama sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyozinduliwa Novemba 25, 2021 na kilele chake kitakuwa Disemba 10, 2021.

Mbunge Janeth Mahawanga, alihitimisha hotuba yake kwa kuwatoa hofu washiriki wa semina hiyo kuwa baada ya mafunzo hayo, kikundi cha Women of Hope Alive hakitawatupa bali kitaendelea kutoa elimu kwa vikundi vingi vichanga na kuvilea mpaka vitakaposimama imara ndani ya Kata zote 102 za mkoa wote wa Dar es Salaam.

#TishaMamaJM
#ItazameDarKiutofauti
#KaziIendeleeNaRSSH

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Janeth Mahawanga akizungumza wakati akifunga Semina ya vikundi vichanga vya Wanawake, iliyoendeshwa na Kikundi cha Women of Hope Alive, kwa ufadhili wa Uholanzi hapa nchini na kufanyika katika ukumbi wa Global hoel, jengo la Mkapa Tower jijini Dar es Salaam, juzi.
Mmoja wa Washiriki wa Semina ya vikundi vichanga vya Wanawake, iliyoendeshwa na Kikundi cha Women of Hope Alive, kwa ufadhili wa Uholanzi hapa nchini akizungumza  wakati wa semina hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Global hoel, jengo la Mkapa Tower jijini Dar es Salaam, juzi.
Washiriki wakiwa kwenye Semina hiyo.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Janeth Mahawanga akiwa na washiriki alipopigwa nao picha ya kumbukumbu  baada ya kufunga Semina ya vikundi vichanga vya Wanawake, iliyoendeshwa na Kikundi cha Women of Hope Alive, kwa ufadhili wa Uholanzi hapa nchini na kufanyika katika ukumbi wa Global hoel, jengo la Mkapa Tower jijini Dar es Salaam, juzi. (Picha zote kwa hisani ya Mbunge Janeth Mahawanga)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages