LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 1, 2021

KANISA HALISI LAMUOMBEA BARAKA TELE RAIS SAMIA KATIKA SAFARI YAKE NCHNI SCOTLAND, NI KATIKA IBADA YA MAMA NA BABA LISHE KULETA 'JIKO JIPYA'.

Rais Samia Suluhu Hassan

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog Tegeta
Kanisa Halisi la Mungu Baba limememuombea kila la kheri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika safari yake ya Glasgow nchini Scotland ambako anahudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa unaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26).

Katika  mkutano huo Rais Samia anatarajiwa kuhutubia mkutano huo, kesho Novemba 2, 2021 ambayo itakuwa ni siku ya pili ya Mkutano huo wa COP 26 unaoanza leo, lengo la Mkutano huo wa COP 26 likiwa ni kujadili jitihada za kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa ili kupunguza joto duniani.

Pamoja na mambo mengine Rais Samia akiwa huko anatarajiwa kukutana na kuzungumza na baadhi Wakuu wa nchi, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa Taasisi mbalimbali pamoja wafanyabiashara wakubwa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi hizo na Taasisi zao.

Kanisa Halisi la Mungu Baba limemuombe Rais Samia na Msafara wake, kila la kheri kwenye safari hiyo katika Ibada maalum iliyofanyika jana, Jumapili kwenye Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta jijiini Dar es Salaam, ikiwahusisha Baba na Mama lishe kwa ajili ya kuleta 'jiko jipya' na kuombea Nchi  isikumbwe na Ukame kwa kukosa mvua kama ilivyotangazwa hivi karibuni na Wataalam.

"Tunamuombea Rais Samia na wale wote walioko katika msafara wake kwa upendo na roho safi, na tunakuombea awe salama huko na arejee salama, atuletee zawadi, na tunapoomba atuletee zawadi, zawadi tunayoomba ni kurejea kwake salama hapa nyumbani tu", alisema Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo anayeitwa Baba Halisi wakati akiongoza Ibada hiyo.

Katika Ibada hiyo iliyohudhuriwa na Uzao (waumini) na Mama na Baba Lishe wengi, Baba Halisi alisema "Mungu Baba tunapomuomba kwa Moyo safi na tukiwa na haki, kila tunachoomba tutapata, hivyo hapa kila aliyeko hapa awe na Moyo safi na kuwa mwenye haki ili Mung Baba atusikie na kuleta mvua yenye kiwango ili kuondosha ukame".

"Ili Mama na Baba lishe waendelee kupika kwa ajili ya Jamii hatimaye tule na tushibe, inahitajika Baraka ya mvua kwa kipimo cha haki kama tunavyosoma katika Yoeli2:23-24.

Katika kipindi hiki tulichonacho wataalamu wa hali ya hewa wametangaza kuwa kutakuwa na ukame na uhaba wa chakula nchini kwa kuwa mvua za vuli zimechelewa kunyesha. Hapa ndipo sote tunapotakiwa kumkimbilia Mungu Baba ambaye ni Chanzo cha Mema na Mazuri ili atupe mvua lakini ni kwa kipimo cha haki. Tunapaswa kutenda haki ndipo tupate Baraka za mvua yenye utoshelevu hatimaye tule na kushiba", Akasisitiza Baba Halisi na kuzitaka Haki hizo akisema;

"Haki ya Kwanza ambayo tunatakiwa kuwa nayo mbele ya Chanzo Halisi (Mungu), aliyekuwepo kabla ya nafsi na roho yoyote ni kumwabudu na kumsujudia yeye tu aliyetuumba kwa jinsi ya ajabu na ya kutisha (Zaburi 139:14).


Haki ya Pili ni kumshukuru kwa yote anayotutendea kila iitwapo leo (Yohana 6:11-13), Haki ya tatu ni kumuita kwa Moyo Mmoja kutokana na tatizo lililoko mbele yetu la Ukame na uhaba wa chakula ambao umekwishatabiriwa na wataalam (Matendo ya Mitume 4:23-24), ili tupate jibu sahihi kutoka kwake.

Haki ya Nne tunayopaswa kuwa nayo ni kukusanyika tukiwa na Moyo Safi (Mathayo 5:8), yaani kuwa na upendo usio na ubaguzi kwa kuwa hakuja kutafuta dini wala dhehebu bali Uzao Halisi juu ya Nchi (Isaya52:5),    Haki ya Tano ni unyenyekevu mbele zake (2 Nyakati7:14-16), ili tukiomba asikie na kutujibu huku jicho lake likiendelea kutuangalia kwa karibu", alisema Baba Halisi na kuendelea kuzitaja haki hizo akisema;

"Haki ya Sita tunayotakiwa kuwa nayo ni kutoa fungu la kumi la mapatoyetu yote, kwa kuwa anasema katika kitabu cha Hagai 1:8-11, kuwa bila kutoa Zaka atakausha Mbingu, Haki ya Saba ni kujitambua kuwa tumependelewa kuwaTaifa Baba, ikiwa na maana ya kuwa chanzo cha Baraka kwa mataifa mengine.

Hii ina maana hatutakiwi kuruhusu ukame na uhaba wa chakula (Mathayo 21:43). Kwa kuwa ndivyo ilivyo, tupeleke matunda mahali alipopachagua (Kumbukumbu12:5-7)".

Baba Halisi alisema, Ibada hiyo ina maana ya Mama na Baba Lishe kuleta nchini 'jiko jipya la kupikia', akimaanisha kuwa siyo jiko la jikoni kama la gesi, la mkaa au kuni bali ni Jiko la nadharia ya kupika Mambo mazuri akisisitiza kuwa na atakayelizima jiko hilo atakufa mwenyewe.

Baba Halisi alisema, kufuatia Ibada hiyo, Mama na Baba Lishe watapata baraka nyingi ikiwemo wateja wengi na kuwataka wawe wepesi katika kutoka huduma kukidhi ongezeko la wateja hao na pia mambo mengi yahusuyo chakula ikiwemo viwanda vitaongezeka.

Ibada hiyo ya jana ni mwendelezo wa Ibada zinazohusisha Jamii ambazo Kanisa Halisi la Mungu Baba limeziendesha jumapili mbili zilizopita ambapo katika Jumapili ya kwanza katika hizo mbili, Baba Halisi alifanya ibada ya kuwabariki Waandishi wa Habari na iliyofuata akafanya Ibada ya Kufuta ajali, ibada ambayo Bodaboda walialikwa na kuihudhiria.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba akinywesha Damu safi (maji yaliyobarikiwa) Mama Lishe alipokuwa akiwabariki Mama na Baba Lishe katika Ibada hiyo jana.

2 comments:

  1. Tunamtukuza Aliyeumba vyote wote na yote, ni Yeye kweli atafuta ukame, ila nasisi wananchi tutilie mkazo kutunza mazingira yetu ili yatutunze. MUNGU BABA AMBARIKI NA
    KUMFANIKISHA RAIS WETU KATIKA MEMA YOTE.

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages