LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 1, 2021

GEKUL AWAPA KONGOLE WAANDAAJI WA OCEAN CITY COMMUNITY MARATHON

 


*

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amewapongeza waandaji wa mashindano ya Riadha ya Ocen City Community Marathon kampuni ya Plus One Events Solutions Co.Ltd kwa kutoa zawadi nono kwa washindi wa mbio hizo.

Mbio hizo zimefanyika leo tarehe 31 Octoba, 2021 jijini Dar es Salaam ambapo mshindi wa kwanza wa Kilomita 21 kwa upande wa wanaume Bw. Alphonce Simbu na Bi. Failuna Matanga kwa upande wa wanawake wamejishindia zawadi ya gari mpya aina ya Passo kila mmoja huku washindi wengine wa Kilomita 21 na 10 wakijishindia fedha taslimu kuanzia Shilingi Milioni mbili na nusu.

Pamoja na zawadi za magari na fedha pia washindi wa kilomita tano kwa upande wa watoto wa kiume na wakike walizawadiwa kiwanja kila mmoja.

"Nimeshiriki mbio nyingi katika mikoa mbalimbali hapa nchini lakini sijawahi kushuhudia washindi wakikabidhiwa zawadi yenye thamani kubwa kama mlivyofanya leo, hongereni sana waandaaji wa mbio hizi" - Mhe. Gekul.

" Zawaidi hizi zitakuwa kichocheo cha kuamasisha wakimbiaji wengi kushiriki riadha hivyo kuchangia kuibua vipaji zaidi" - Mhe. Gekul

Pamoja na kuamasisha michezo, mashindano ya Ocen City Community Marathon yamelenga kuchangisha fedha kwa ajili ya Bima ya Afya kwa watoto yatima ambapo Mhe. Gekul amesema Serikali itaendelea kuwaunga mkono waandaaji wa mashindano hayo na kutoa wito wa kuhakikisha kuwa mashindano hayo yanakuwa endelevu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages