LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 8, 2021

KAMATI YA BUNGE YA KAMATI YA MADINI NA NISHATI WAPIGWA MSASA KUHUSU MRADI WA KABANGA NICKEL+video

Waziri wa Madini, Dotto Biteko akifafanua jambo wakati wa semina ya wizara kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Madini na Nishati kuhusu mradi wa madini wa Kabanga Nickel , Ngara mkoani Kagera. Kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Seif Gulamali.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Madini na Nishati wamepigwa msasa katika semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Mradi mpya wa uchimbaji madini aina ya Nickel wa Kabanga Nickel uliopo wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera.
Semina hiyo imeendeshwa na wataalam wa Wizara ya Madini jijini Dodoma, ambapo wameelezwa kuwa ukianza kuzalisha utakuwa unaliingizia Taifa zaidi ya sh. bilioni 500 kwa mwaka. Aidha, zimetengwa zaidi ya dola milioni 50 kwa ajili ya kulipia fidia kwa wananchi pamoja na kujenga miundombinu.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Seif Gulamali. (katikati) akiongoza kikao cha semina hiyo.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa katika semina hiyo.



PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Seif Gulamali, Waziri wa Madini, Dotto Biteko na Mbunge wa Ngara, Ndaisaba Ruhoro wakielezea yaliyojiri kwenye semina hiyo na jinsi wananchi wa Ngara walivyojiandaa kwa kuupokea mradi huo kwa furaha...
 

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages