Ujenzi na uwekaji wa baadhi ya MIUNDOMBINU ya Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Mugango
WANANCHI na VIONGOZI wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kutoa SHUKRANI NYINGI kwa SERIKALI yao inayoongozwa na MHE SAMIA SULUHU HASSAN, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa KUWAPATIA FEDHA ZA COVID-19 kwa ajili ya usambazaji maji ya bomba vijijini mwao.
*Tsh MILIONI 500 zimetolewa kwa ajili ya kusambaza maji ya bomba kwenye Vijiji 3 vya: KANDEREMA, BUGOJI na KABURABURA. Mradi huu wa maji kutoka Ziwa Victoria tayari unatekelezwa, na chanzo cha maji kiko Kijijini Suguti, Kata ya Suguti.
Mradi huu unatekelezwa wa RUWASA, Musoma Vijijini
*Tsh MILIONI 300 zitatumika kusambaza maji kwenye Vijiji 2 vya: KURWAKI (Kata ya Mugango) na KIRIBA (Kata ya Kiriba). Huu nao ni Mradi wa maji ya Ziwa Victoria na chanzo chake kiko Kijijini Kwibara, Kata ya Mugango
Mradi huu wa Vijiji 2 utakuwa sehemu ya Mradi Mkuu wa Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama.
TAARIFA ya utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari- Butiama, utakaogharimu Tsh BILIONI 70, itatolewa hivi karibuni.
Taarifa kutoka:
*Ofisi ya RUWASA
Musoma DC
*Ofisi ya Mradi wa
Mugango-Kiabakari-Butiama
*Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇