LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 25, 2021

ZIARA YA MBUNGE KILAVE KUKAGUA MIRADI JIMBONI TEMEKE YAPAMBA MOTO, ATEMBELEA KATA YA KILAKALA, LEO

Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akimuonyesha na kumweleza ubora wa mashine ya 'Photocopy' Katibu wa CCM Kata ya Kilakala Issa Chacha (Wapili kushoto), kabla ya kumkabidhi mashine hiyo ili naye amkabidhi rasmi Mkuu wa shule ya Msingi Kilakala (kushoto), alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Jimbo kati ya mwaka 2020-21 katika Kata ya Kilakala, leo. Amesema Mashine hiyo ilinunuliwa kwa zaidi ya Sh. milioni moja kutoka Mfuko huo ili kuiwezesha shule hiyo kurahisisha shughuli zake za kurudufu nyaraka mbalimbali.
Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akimkabidhi mashine hiyo ya Katibu wa CCM Kata ya Kilakala Issa Hamisi Chacha (Wapili kushoto), ili naye amkabidhi rasmi Mkuu wa shule ya Msingi Kilakala (kushoto).
 Kisha Mbunge Mama Kilave akasaini kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Kilakala.

Kisha akatoka Ofisini kwa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kwa ajili ya kwenda kukagua eneo ambalo litajengwa majengo ya madarasa zaidi kutokana na juhudi za Mbunge huyo.
Mkuu wa shule ya Msingi Kilakala akimuongoza Mbunge Kilave na Msafara wake kwenda kukagua eneo hilo.

"Kwa hiyo ni mpaka kuleee, ni eneo la kutosha", akisema Mbunge Kilave wakati akionyeshwa eneo hilo na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Kilakala.
Shule hiyo ya Kilakala inapakana na shule nyingine ya Msingi ya Kigunga. Mbunge Kilave akionyeshwa jiwe la mpaka wa shule hizo alipokuwa katika ziara hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akifurahi na Wanafunzi wa darasa la Pili katika Shule ya Msingi Kigunga alipozungumza nao wakati wakiwa mapumziko alipotembelea shule hiyo, leo.

Mbunge wa Temeke Dorothy Kilave akiwasalimia baadhi ya Walimu wa shule ya Msingi Kigunga, alipotembelea maeneo mbali mbali ya shule hiyo, leo Novemba 24, 2021, akasema "Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" wakajibu "Kazi Iendelee".
Mbunge wa Jimbo la Temeke Jijini Dar es Salaam Dorothy Kilave akizungumza na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kigunga Jane Barongo (kushoto), alipotembelea shule hiyo, katika ziara yake. Mbunge huyo alimhakikishia mwalimu huyo kuwa ahadi yake ya shule hiyo kupata mashine ya 'Photocopy' ipo palepale na itatekelezwa kabla ya mwishoni mwa Disemba mwaka huu.

Kisha akasani kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mwalimu Mkuu huyo. Kulia ni Msaidizi wake.
Mbunge wa jimbo la Temeke Dorothy Kilave akisalimiana na  'mdau' wake kijana aliyemkuta akikusanya machupa matupu ya maji katika eneo la Shule ya Msingi Kigunga wakati akiwa katika ziara yake hiyo katika Kata ya Kilakala.

"Mimi nakufahamu sana, Wewe ni Mbunge wetu wa Temeke Mama Kilave, Mimi ni Mdau wako", akasema kijana huyo.

Kisha akasalimiana na Wanafunzi wa darasa la pili kwenye shule hiyo👇

"Watoto nani anajua jina la Rais wa jamhuri ya Mungano wa Tanzania?" Mbunge Kilave akawauliza watoto hao nao wakanyoosha vidole na kujibu "Ni Mheshimiwa Samiaaa".
Mbune wa Jimbo la Temeke Mama Dorothy Kilave akikagua kazi inayoendelea kufanywa katika kuboresha madawati katika shule hiyo ya Msingi Kigunga. Kazi hiyo inafanyika kupitia mradi wa EP4R.

Mbunge wa Jimbo la Temeke Mama Dorothy Kilave akipata maelezo kuhusu mradi huo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Jane Barongo. 

Baada ya kuondoka kwenye shule hiyo Mbunge Kilave akapiga shoto-kulia hadi kwenye Zahanati ya Kilakala kuona hali ya mambo na kukagua eneo litakalojengwa majengo zaidi kutanua zahanati hiyo👇

Mbunge kilave akiwa ofisini kwa Mganga Mfawidhi Msaidizi katika Zahanati hiyo ya Kilakala Daktari Edinithon Maro.
Kisha akatua Chumba cha Maabara, Hapa akipata maelezo kuhusu utendaji kazi wa Maadara hiyo kutoka kwa Mganga Mfawithi wa Zahanati hiyo Daktari Acklace Mlau (kushoto).

Mbunge wa Temeke Dorothy Kilave akiongozwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanari hiyo Daktari Acklace Mlau kukagua maeneo mbalimbali ya utoaji huduma katika Zahanati hiyo.
"Hapa ni eneo la Huduma ya Kliniki ya Mama na Mtoto", akasema Daktari Mlau kumwambia Mbunge Klave.
"Na hapa ni chumba cha kupumzisha wagonjwa, tumejitahidi kupatunza pawe nadhifu mda wote", akasema Daktari Mlau kumweleza Mbunge Kilave.
"Na huo unaouona kulia kwangu ni mtungi tuliopatiwa kwa ajili ya Wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji ikiwemo itokanayo na Covid 19, lakini tunashukuru ni kwa muda mrefu sasa hatuwapata wagonjwa wenye changamoto hiyo", akasema Daktari Mlau kumwambia Mbunge Kilave.
Kisha Daktari Mlau akampeleka Mbunge Kilave kwenda eneo lingine.

"Mheshimiwa Mbunge, hapo ndilo eneo tunalotupa na kuteketeza taka ngumu na zenye madhara kwa afya za binadamu", akasema Daktari Mlau kumweleza Mbunge Kilave walipokuwa wakipita eneo hilo.
Kisha Mbunge Kilave na Ujumbe wake wakafika kwenye Kituo Maalum cha kupia na kutoa Huduma ya magonjwa ya Ukimwi na Kifua Kikuu kwenye Zahanati hiyo. "Kwa hiyo eneo lile ndipo kutajengwa majengo mapya ili kuitanua Zahanati hii? Ohh, ni eneo la kutosha sana, Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulipatia jimbo letu Sh. milioni 250 kwa ajili ya upanuzi wa Zahanati hii. Naomba ujenzi utakapokamilika huduma za Mama na mtoto zitolewe kwa saa 24", akasema Mbunge Kilave kumweleza Daktari Mlau.
Baada ya kutoka katika Zahanati ya Kilakala Mbunge Kilave akatinga katika Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata hiyo ya Kilakala na kuanza kwa kusaini kitabu cha Wageni. Kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Rajabu Ramadhani.

Kisha Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave chumba cha kutolea chanjo ya huduma ya Uviko 19 katika Ofisi hiyo ya Afisa Mtendaji. 

Kisha Mbunge Kilave akaenda Ofisi ya CCM Kata ya Kilakala kuhitimisha ziara kwa kufanya majumuisho👇

Katibu wa CCM Kata ya Kilakala Issa Hamisi Chacha akizungumza kufungua kikao cha Majumuisho.
NAfisa Mtendaji Kata ya Kilakala Rajabu Ramadhani akizungmza kabla ya kumkaribisha Mbunge Kilave kuzungumza.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho cha kuhitimisha ziara hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Temeke Mama Dorothy Kilave akizungumza katika Kikao cha Kuhitimisha ziara yake katika Kata ya Kilakala kukagua miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika Kata hiyo kupitia Mfuko wa Jimbo lake.

1 comment:

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages