LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 25, 2021

WIZARA YA AFYA YASHIRIKISHA SEKTA BINAFSI KUONGEZA KASI MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO-19+video

 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi akielezea mkakati wa kuzishirikisha asasi za kiraia na sekta binafsi katika mapambano dhidi ya UVIKO-19 katika mkutano na asasi hizo uliofanyika leo Oktoba 25, 2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji  na Tathmini -Mpango wa Taifa wa Chanjo, Dkt Mwendwa Mwenesi akitoa mada wakati wa mkutano huo.
Dkt Marz Kitama akiwasilisha mada kuhusu mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Katibu Mkuu, Profesa Makubi akifafanua jambo katika mkutano huo.
Baadhi ya wadau wakisikiliza kwa makini mwenendo wa mkutano huo.
Katibu Mkuu, Profesa Makubi akiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka asasi ya kiraia na sekta binafsi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


SERIKALI imeamua kuzishirikisha asasi za kiraia na sekta binafsi kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya UVIKO-19. Hilo limeabainishwa wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi katika mkutano wa kuweka mikakati ya pamoja na asasi hizo kukabiliana na UVIKO-19 jijini Dodoma leo. Profesa Makubi mesema wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la kuchanja chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 ambapo watu Milioni 1 wamechanja chanjo ya Jonson Jonson (JJ) huku watu 20,000 wakiwa tayari wamesha chanja chanjo mpya ya Synopharm . Amesema kuwa chanjo ya Synopharm ni chanjo ambayo mtu anatakiwa kuchanja mara mbili ndani ya siku 28 ili kinga yake iwe imara zaidi na ndio dozi kamili ya chanjo hiyo. " Hapa naomba kusisitiza kitu kwa wananchi kutorudia kuchanja chanjo mara mbili kama wewe umesha chanja chanjo ya Jonson Jonson usirudie tena kuchanja chanjo hii mpya ya Synopharm," amesisitiza Profesa Makubi. Na kuongeza kusema "leo tuko hapa katika kikao hiki tumekutana na sekta zisizokuwa za kiserikali pamoja na NGos kwani wao wako tayari kushirikiana na serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo ya UVIKO 19 kwa kuhakikisha wanawahamasisha na kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa uchanjaji wa chanjo ya UVIKO 19," amesema . Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Tamisemi anayeshughulikia Afya Dkt Grace Magembe amesema wao kama Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi wamedhamilia na kuhakikisha kazi ya uhamasishaji inakwenda vizuri " Sisi Tamisemi tunashughulikia watu wengi hivyo baada ya kufika kwa chanjo hapa nchini tuliandaa mpango shirikishi kwa kuongea na wakuu wa mikoa na viongozi wa dini kueleza wananchi umuhimu wa uchanaji wa chanjo ya UVIKO 19 na katika hili tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa," Na kuongeza"Mafanikio ya wananchi kuchanja chanjo ya UVIKO 19 yapo na yanaonekana kwa kutumia viongozi wa serikali Dini na viongozi wa kimila watu hawa maetusaidia na hatimaye wananchi wamejitokeza kuchanja," amesema Dkt Magembe.. Naye Lilian Badi Mwenyekiti wa Baraza la Taifa NGos amesema kama asasi za kirai wako tayari kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO 19.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video hapa chini ujue kilichozungumzwa katika mkutano huo....Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages