LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 27, 2021

WIZARA YA AFYA YAANZA KUFANYA TAFITI SITA ZA VIRUSI VYA CORONA




Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof Abel Makubi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Oktoba 27, 2021.

.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA



WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, imeanza   kufanya tafiti za kitaalam kuhusu Virusi vya Corona  kwa kufanya tafiti sita (6).

Tafiti hizo ni  kuhusu tabia za virusi vya Corona kwa kuangalia askari wa kinga mwili (antibodies), uelewa, mtazamo na utendaji,utafiti wa kimatibabu, kuchunguza mpangilio wa vinasaba,hali ya kimelea kubadili hali/vinasaba vyake vya awali na utafiti wa tiba asili.

Hayo yameelezwa  leo Oktoba 27,2021 Jijini Dodoma na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof Abel Makubi wakati akizungumza  na Waandishi wa habari.

Katibu Mkuu huyo amesema  kuwa kati ya Shilingi, bilioni 466.781, Shilingi  bilioni 259.228 zitasimamiwa na Wizara hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi iliyoko chini yake pamoja na Taasisi na Hospitali.

Amesema  Shilingi 207.643 zitasimamiwa na OR - TAMISEMI kwa ajili ya utekelezaji miradi ya afya iliyoko chini ya OR - TAMISEMI ikijumuisha vituo vya kutolea huduma za afya katika ngazi ya Msingi (Halmashauri) kuanzia hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati.

Amesema ili kufanikisha tafiti hizo,Wizara imejipanga kujenga na kukarabati Hospitali sita za Rufaa za Mikoa ya Lindi, Songea, Kigoma, Mtwara (Ligula), Tabora (Kitete), Katavi, Ukerewe na Taasisi ya afya ya akili Mirembe na kwamba matokeo ya tafiti hizo yatawezesha Serikali kufahamu aina ya kirusi kilichopo nchini ili kufanya vipimo na kutoa chanjo.

Amefafanua kuwa hatua hiyo pia itasaidia  kufahamu sababu za muitikio mdogo  wa jamii katika kupata chanjo ya UVIKO - 19 hivyo kuishauri Serikali njia sahihi ya kuongeza muitikio; kufahamu ufanisi wa dawa za asili katika kupambana na UVIKO - 19 na kuishauri Serikali; Kufahamu madhara ya UVIKO - 19 kwa wagonjwa wanaopata maambuki; kufahamu  viambata vilivyopo kwenye dawa za asili ambavyo vinasababisha utibabu wa korona na kufanya ugunduzi wa chanjo dhidi ya UVIKO-19 .

Amesema uwekezaji huo unategemewa kuwa na faida kwa  kupunguza vifo vya wagonjwa kwa asilimia 20-40% ndani ya vituo vya afya, kuimarisha huduma za maabara, mionzi na tiba mtandao; itakayogharimu Shilingi bilioni 111.5 ambayo itasaidia ugunduzi wa haraka wa magonjwa mbalimbali,kupunguza rufaa kwenda Hospitali ya Taifa na kuimarisha huduma za chanjo dhidi ya UVIKO - 19 , elimu ya afya kwa umma dhidi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo itakayogharimu Shilingi bilioni 43.2. hivyo kuwezesha kuwakinga Wananchi wengi dhidi ya vifo vinavyohususiana na UVIKO-19.

"Kupitia fedha hizi tunaimarisha miundombinu katika vituo vya kutolea huduma za Afya itakayogharimu Shilingi bilioni 41.8 na hivyo kupanua na kuboresha huduma za kibingwa katika ngazi ya mikoa na Kanda lakini pia kufanya tafiti za kitaalam kuhusu Virusi vya Korona pamoja na kuwajenga uwezo watoa huduma za Afya itakayogharimu Shilingi bilioni 15.9. 2.1,"amesema.

Prof.Makubi pia ametumia nafasi hiyo kueleza namna malengo hayo yanavyotekelezwa ambapo amesema  Sekta hiyo imeaza michakato ya  kukarabati na kujenga majengo ya matibabu ya dharura (EMD) 102, vitengo vya wagonjwa wanaohitaji uangallizi maalum (ICU) 67 na kusimika vifaa vyake.  

Aidha amesema ,Hospitali ya Taifa itakarabati ICU 2, Hospitali Maalum na Ubingwa Bobezi (ICU 5 na EMD 1); Hospitali za Kanda (ICU 5 na EMD 4); na katika ngazi ya mikoa na Halmashauri (ICU 30 na EMD 80) chini ya OR TAMISEMI.

"Fedha hizi poa zitaimarisha mfumo wa rufaa kwa kununua na kusambaza magari 253 ya kubebea wagonjwa, kati ya magari hayo magari 20 ‘advanced ambulances’ yatapelekwa katika viwanja vya ndege vya Julius Nyerere (1), KIA (1), Mwanza Airport (1), Hospitali ya Mzena (1), Hospitali za Rufaa za Mkoa (8), Hospitali za Kanda (6), Hospitali Maalum na Ubingwa Bobezi (5);

Prof.Makubi ameeleza kuwa sekta hiyo inafanya mambo kadhaa kuimarisha uwezo wa  Maabara ya Taifa na Maabara nyingine nchini ili kupima na kutoa majibu ya sampuli kwa wakati na kununua  vitendanishi vya kupima sampuli katika maabara za mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Mara, Dodoma, Arusha (Mt. Meru), Tanga na Mtwara .  

“Ili kuwezesha utoaji wa majibu ya vipimo vya sampuli kwa wakati,

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages