LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 27, 2021

BABA HALISI AWAFUNDA BODABODA KUWA WAAMIFU, AWAAMBIA TABIA HIYO INALIPA, AMBARIKI RAIS SAMIA NA WASAIDIZI WAKE

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Tegeta
Baba Halisi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba lenye Makao yake Makuu Tegeta jijini Dar es Salaam, amewafunda waendesha Bodaboda wawe wema kwa abiria wao, akiwaambia kuwa kufanya mwenendo huo kutawafanya kupata faida zaidi kuliko wakiwatendea ya hovyo wateja hao.

Baba Halisi amewafunda katika Ibada Maalum ya kufuta ajali, ambayo iliandaliwa na Kanisa hilo na kuwaalika Bodaboda ambayo ilifanyika juzi, Jumapili, Oktoba 24, 2021 (12 Eluli, Vol2), na kuhudhuriwa na vijana wa Bodaboda zaidi ya 30.

 

Katika Ibada hiyo, Baba Halisi alisema, baada ya Ibada hiyo sasa Bodaboda hao wafanye kazi yao kwa Uaminifu wataona ajali zilizokuwa zikiwaandama zimefutika na vipato vyao vitokanavyo na kazi hiyo vitakuwa vikubwa zaidi.

 

Alienda mbali zaidi kwa kuwapa mfano, akisema katika nchi moja alikuwepo mwendesha pikipiki (bodaboda), siku moja abiria wake akasau kifurushi cha pesa kiasi cha dola 50,000 za Kimarekani, huyo Bodaboda akaamua kumtafuta.

"Yule kijana akawa anahangaika kuwauliza watu, jamani kuna mtu kasau furushi lenye pesa, namtafuta nimrejeshee, mmemuona? Wale watu wakawa wanamcheka huyo bodaboda, wakimwambia wewe mjinga sana, Mungu amekupatia hizo pesa, si uzichukue tu uondokane na ufukara?", akasema Baba Halisi, huku baadhi ya Uzao (waumini) na Bodaboda waliokuwa katika Ibada hiyo wakicheka na wengine wakishangaa.

Baba Halisi akaendelea kusimulia kisa hicho, akasema, " Yule Bodaboda aliendelea kumtafuta mpaka akampata abiria wake, alipompata yule Bwana akafurahi sana akachukua Dola 2,500 akampatia yule kijana.

 

Baadaye Rais wa Nchi ile akapata taarifa, akamwita Ikulu, akamwambia kijana kuanzia sasa wewe utakuwa Balozi wa Uaminifu wa nchi hii na kwa kuwa nimekuteua nitakuwa nakulipa mshahara kila mwezi, Pia Rais yule akampa huyo kijana pikipiki zingine mbili.

"Sikilizeni wanangu, sasa nimeshawabariki kafanyeni kazi yenu kwa uaminifu, watendeeni vema abiria wenu. mimi mwenyewe hapa nafanyakazi kwa uaminifu natumia sauti yote kwa uaminifu bila kuibana. Nakuambieni kweli, uaminifu unalipa". Baba Halisi akasema huku akisistiza, "Uaminifu unalipa".

Mwishoni mwa Ibada hiyo Baba Halisi akatuma Bodaboda na wenye magari wagawiwe kadi ambazo watabandika kwenye eneo la namba za bodaboda au magari yao

Mapema akianza ibada hiyo, alimuombea Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa na viongozi wote wanaomsadia Rais katika ngazi zote tangu mikoa, Wilaya, Kata hadi Vijiji, vitongoji na mitaa.

Simuliza ya Ibada hiyo kwa picha👇

"Heri Heri", Baba Halisi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba  akisema kuwasalimia Uzao (Waumini) mwanzoni mwa Ibada maalum yakufuta ajali, ambayo Bodaboda walialikwa kuhihudhuria, juzi, Jumapili, Oktoba 24, 2021 (12 Eluli, Vol2), kwenye Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta jijini Dar es Salaam.
Baba Halisi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba akipeperusha kitambaa cheupe kuungana na Uzao (Waumini) kushangilia baada ya kufungisha ndoa Uzao mwanzoni mwa Ibada maalum yakufuta ajali, ambayo Bodaboda walialikwa kuhihudhuria, juzi, Jumapili, Oktoba 24, 2021 (12 Eluli, Vol2), kwenye Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta jijini Dar es Salaam.
Baba Halisi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba akiendelea kupeperusha kitambaa cheupe kuungana na Uzao (Waumini) kushangilia baada ya kufungisha ndoa Uzao mwanzoni mwa Ibada maalum yakufuta ajali, ambayo Bodaboda walialikwa kuhihudhuria, juzi, Jumapili, Oktoba 24, 2021 (12 Eluli, Vol2), kwenye Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaka Halisi wa Uzao.
Baahi ya Uzao (Waumini) nao wakishanagilia baada ya Baba Halisi kufungisha ndoa Uzao mwanzoni mwa Ibada maalum yakufuta ajali, ambayo Bodaboda walialikwa kuhihudhuria, juzi, Jumapili, Oktoba 24, 2021 (12 Eluli, Vol2), kwenye Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta jijini Dar es Salaam.
Mama Halisi wa Uzao akiungana na Uzao wengine kushangilia tukio hilo. Kulia ni Dada Halisi wa Uzao.
Mwimbaji wa kwaya ya Kanisa Halisi la Mungu Baba akiongoza kuimba wimbo wa kumtukuza Mungu Baba wakati wa Ibada hiyo.
Uzao wakiiba wimbo huo wa kumtukuza Mungu Baba wakati wa Ibada hiyo.
Uzao wakicheza kwa staili ya kipekee wimbo huo wa kumtukuza Mungu Baba wakati wa Ibada hiyo.
Siyo Gwaride, bali ni Uzao wakicheza kwa staili ya kipekee wimbo huo wa kumtukuza Mungu Baba wakati wa Ibada hiyo.

Uzao akijaribu kufikisha kilele chake cha mwisho cha kucheza wakati wimbo huo wa kumtukuza Mungu Baba ulipokuwa ukiimbwa
Uzao wakiendelea kucheza wimbo huo wa kumtukuza Mungu Baba

Uzao akiamua kumbeba uzao mwenzake baada ya kumalizika wimbo huo wa kumtukuza Mungu Baba

 

Kisha Baba Halisi akaendelea kuongoza Ibada hiyo

👇


Baba Halisi akifafanua baadhi ya maandiko kutoka katika Kitabu chake.
Uzao akinukuu maafundishi ya Baba Halisi, huku akiwa amempakata mtoto wake.
Uzao wakinukuu maafundishi ya Baba Halisi
"Wanangu baada ya Ibada hii, mtaona ajali zilizokuwa zikiwaandama Bodadoda zinafutika, na mkafanye kazi kwa uaminifu, Uaminifu unalipa", Baba Halisi akiwaambia Bodaboda waliohudhuria Ibada hiyo.
Vijana Bodaboda waliohudhuria Ibada hiyo ya Kufuta ajali wakimsikiliza Baba Halisi kwa utulivu
Vijana Bodaboda waliohudhuria Ibada hiyo ya Kufuta ajali wakiendelea kumsikiliza Baba Halisi kwa utulivu

Vijana Bodaboda waliohudhuria Ibada hiyo ya Kufuta ajali wakionyesha kuyatafakari mafundisho ya Baba Halisi kwa utulivu.

 

Kisha ukaimbwa wimbo wa Kumtukuza Chanzo Halisi

👇

Uzao akiimba wimbo wa Kumtukuza Mungu Baba huku akicharaza kinada wakati wa Ibada hiyo. Pembeni yake ni Mwanamuziki nguli King Maluu akiungurumisha 'Domo la Bata'.

Wimbo huo ukawa unasikiza wakati Vijana wa Bodaboda waliohudhuria Ibada hiyo wakipata soda👇

Kuhani Faida akiwagawia soda vijana wa Bodaboda
Kijana wa Bodaboda 'akipoza koo' kwa soda walizopewa Baba Halisi

Vijana wa Bodaboda wakiendelea kunywa soda👆. Huku wimbo wa Kumtukuza Mungu Baba ukiendelea kuungurumishwa na kwaya waliokuwa wakiimba kwa hisia za kutosha.👇

Kisha Baba Halisi akaendelea na Ibada👇
Baba Halisi wa Uzao akiendela na Ibada hiyo kuwabariki Baodaboda.
Bodaboda wakipokea baraka za Baba Halisi
Baba Halisi akibariki kwa kunyunyiza Damu Safi (Maji yenye baraka)
Makuhani wakigawiwa vitabu. Baadaye Baba Halisi akitangaza kuwapa mapumziko ya siku tano, kila Kuhani akiende nyumbani kwao kuonana na Wazazi wake lakini akirudi aje na picha kuonyesha huyo na Mzazi wake.
Baba Halisi wa Uzao akiwakaribisha wenye zawadi kwa maharusi.
Maharusi wakipewa zawadi
Maharuzi Kuhani Hema akiwa na mkewe Upendeleo Halisi wakati wakisubiri kuzawadiwa na uzao. Kulia ni Kuhani Faida.
 
Kisha Kuhani wa Utawala wa Amani kutoka Kituo cha kanisa Halisi kilichopo Marekani, Kuhani Peace Baraka akizungumza baada ya kupewa nafasi na Baba Halisi 👇



Kuhani Peace akawatambulisha pia Kuhani wa Kituo cha Kanisa Halisi kilichopo marekani na mkewe

Kuhani wa Kituo cha Kanisa Halisi kilichopo marekani na mkewe
Kuhani kutoka Ilala nayeye akapewa nafasi ya kusalimia Uzao kwenye Ibada hiyo
Kuhani Sauti akiwa kwenye Ibada hiyo
Kuhani akiimba wimbo wa Kumtukuza Mungu Baba
Uzao wakishangilia kufurahia ibada hiyo
Bodaboda wakipewa stika za kubandika kwenye bobaboda zao
Maharusi wakitangulia kutoka Kanaisani kwa ruksa ya Baba Halisi

Maharusi wakitangulia kutoka Kanaisani kwa ruksa ya Baba Halisi.
Maharusi wakitangulia kutoka Kanaisani kwa ruksa ya Baba Halisi. Kulia ni baadhi ya Pikipiki za vijana wa Bodaboda walioshiriki ibada hiyo
Uzao akitoka Kanisani baada ya Ibada hiyo, huku akiwa amejpamba kwa skafu ya Bendera ya Taifa.

1 comment:

  1. Chanzo Halisi Ni wa wote walio umbwa,atukuzwe,ahimidiwe,asujudiwe na apewe sifa,Imekuwa.

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages