LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 27, 2021

MAKINDA AZIOMBA ASASI ZA KIRAIA KUSHIRIKI KIKAMILIFU UHAMASISHAJI WA SENSA+video


Kamisaa wa Sensa, Spika mstaafu Anne Makinda akizungumza wakati wa Kongamano la Wiki ya Azaki jijini Dodoma leo Oktoba 27, 2021. ambapo ameziomba Asassi za kiraia kushiriki kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi Siku ya sensa mwakani.


Wadau wa AZAKI wakitoa ushauri na kuuliza maswali kuhusu sens








Afisa Mtwakwimu Mwandamizi  wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),  akielezea kuhusu umuhimu na faida za sensa katika m,aendeleo ya nchi.

Anne Makinda akiteta jambo na Kiongozi wa ittACT Wzalendo Zitto Kabwe 
Ane Makinda akiondoka kwenye Kongamano huku akisindikizwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Foundation foro Civil Society, Frncis Kiwanga

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA




Na Mwandishi Wetu Dodoma

ASASI za kiraia nchini (AZAKI) zimetakiwa kushirikiana na Serikali kuhamasisha Wananchi kushiriki kikamilifu Katika zoezi la Sensa ya watu na makazi lililopangwa kufanyika ifikapo  Agosti 2022. 

Hayo yameelezwa mapema leo na Kamisaa wa Sensa kwa mwaka huu,Spika mstaafu Anne Makinda wakati akitoa mada ya uelimishaji na uhamasishaji  wa masuala ya sensa kwa Asasi za Kiraia Katika Mkutano wa wiki ya AZAKI unaoendelea Jijini hapa.

Mh.Makinda ameeleza kuwa umuhimu wa sensa unagisa Kila nyanja hivyo ni wajibu kwa kila mtanzania kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa.

"Sensa ni muhimu na inafanyika Kila baada ya miaka kumi,nyinyi watu wa AZAKI ni wadau namba moja ,tunatakiwa kutoka kwenye uchumi wa Kati tuendende zĂ idi tufanane na wenzetu,"ameeleza.

Amesema Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012 hivyo Sensa ya mwaka huu  itakuwa ni sensa ya sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.

"Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum,kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, 

kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi. Takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo,"amefafanua Makinda.

Kwa umuhimu huo,Kamisaa huyo wa sensa ameeleza upekee wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kĂşwa utazingatia taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimalimali.

"Taarifa za sensa zitawezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira,msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia,takwimu hizi zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa,"amefafanua.

Kwa upande wake amesema sensa ya mwaka 2022 kama zilivyo sensa zilizopita itatumia aina mbili kuu za madodoso ambazo ni dodoso refu litakalotumika kuhoji asilimia 30 ya maeneo yote ya kuhesabia watu na Dodoso fupi litakalotumika kuhoji kwenye asilimia 70 ya maeneo yote ya kuhesabia watu.

Ameyataja madodoso mengine kuwa ni  la Taasisi ambalo ni mahsusi kwa ajili ya wasafiri, waliolala mahotelini/nyumba za wageni, na waliolazwa hospitalini na dodoso la Wasio na Makazi maalum ambalo ni mahsusi kwa watu wote wanaolala maeneo yasiyo rasmi, kwenye baraza za majengo mbalimbali, kwenye madaraja na maeneo mengine.

"Utekelezaji wa sensa ya watu na makazi hufanyika katika awamu kuu tatu kuu ambazo ni kipindi kabla ya kuhesabu watu, wakati wa kuhesabu watu na kipindi baada ya kuhesabu watu,"amesisitiza.

Licha ya hayo Mtakwimu huyo Mwandamizi amefafanua maswali yatakayoulizwa wakati wa sensa ya Watu na Makazi mwaka huu huku akieleza kiwa moduli kumi na nne zitatumika kukusanya taarifa za watu na makazi yao nchi nzima.

 "Maswali hayo ni tarifa za kidemografia (umri, jinsi, uhusiano, hali ya ndoa, uraia, Maswali yanayohusu ulemavu;tarifa za Elimu;maswali ya uhamaji, pamoja na taarifa za Watanzania wanaoishi nje ya nchi,mengine ni maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa (vitambulisho vya NIDA, Mzanzibari mkazi, cheti cha kuzaliwa, hati ya kusafiria, na leseni ya udereva),shughuli za kiuchumi na umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA,"amesema.

Aidha ametaka maswali mengine yatakayoulizwa kipindi cha sensa  kuwa ni tarifa za uzazi na vifo vilivyotokea ndani ya kaya,vifo vitokanavyo na uzazia,hali ya nyumba za kuishi na umiliki wa rasilimali mbalimbali,maswali ya kilimo na mifugo pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii.

"Tunaomba AZAKI mshiriki kikamilifu kuelimisha jamii tufikie malengo,sisi kama Ofisi ya Takwimu tumejipanga vizuri kwa kutumia rasilimali chache zilizopo ili kukamilisha kwa wakati shughuli zote za maandalizi ikiwamo kazi ya utengaji wa maeneo ya kuhesabia watu katika ngazi ya kitongoji na mtaa ambayo ndiyo msingi wa kufanikisha sensa kwa ubora,"ameeleza.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video ujue yaliyojiri kwenye kongamano hilo...
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages