LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 27, 2021

MAMA MASUNGA AFUNGA KONGAMANO LA WANAWAKE 600, MLIMA WA MOTO, AWAASA KUENDELEA KUIOMBEA TANZANIA IZIDI KUPIGA HATUA

Na Mwandishi Maalum
Mwenyeiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mama Florence Masunga  amewaasa kuendelea kuiombea Tanzania iendelee kuwa na amani na utulivu chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hasaan ili iendelee kupiga hatua kimaendeleo na kijamii.

Mama Masunga amewaasa Wanawake hao alipokuwa akizungumza wakati akifunga kongamano la Wanawake 600 wa Kanisa la Mlima wa Moto lililopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.

Katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Dk. Rose Rwakatare na Askofu wa Kanisa Hilo Mama Rose Mgeta, Mama Masunga aliwaasa pia Wanawake hususani Waslioshiriki Kongamano hilo kuchanjwa chanjo ya Uviko 19 kwa kuwa familia inapopata ugojwa huo Mama ndiye anaewajibika kila mahala hata kwa kulala hospitali iwapo baba au mtoto atadhurika
 
Mama Masunga aliwapongeza wanawake waliohudhuria Kongamano hilo ambalo lilifanyika kwa siku saba mfululizo na amepongeza pia Dk. Rose Rwakatare kwa kuweza kusimamia yale yote yalioasisiwa na Marehemu Dk. Getrude Rwakatare ikiwemo Kongamano hilo alianzishe katika mikoa yote nchini miaka kumi iliyopita.

Aidha Mama Masunga aliwapongeza  Wanafamilia ya marehemu Dk. Getrude Rwakatare kwa kuendelea kusimamia mambo yote mazuri aliyoyaacha mama yao na pia amewaasa waendelee kuwa wamoja kama Bwana Yesu Kristo alivyosema kwamba amewaachia umoja.

Akizungumza kwenye ufungaji Kongamano hilo Rutta Rwakatare aliwaasa Kinababa nao waendelee kusimama na umoja wao walioanzisha Kanisani hapo uwe na nguvu kama wa Kinamama hao walivyo na nguvu hadi Sasa.

Kwa uapnde wake, Askofu Rose Mgeta aliwashukuru wahudhuriaji wa Kongamano hilo na kuwashukuru kwa kuwapa mahitaji mbalimbali wale watu wahitaji na msaidizi wa Askofu Rutta Rwakatare aliongoza kuwapatia wahitaji fedha pamoja na vyakula mbalimbali kama ilivyokuwa toka kongamano hilo liasisiwe na marehemu Dk. Getrude Rwakatare,

Dk. Rose Rwakatare ambaye ni mlezi wa Kanisa hilo naye amewasisitiza Kinmama hao wajitokeze kwa wingi kwenye sensa ya watu na makazi itakayofanyika Oktoba mwakani katika mchi nzima, waonyeshe ushirikiano na kuunga mkono serikali chini ya Rais Samia,

Mama Masunga akiwa katika baadhi ya Matukio katika picha yaliyojiri kwenye ufungaji Kongamano hilo👇

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa dar es Salaam, Mama Florence Masunga (kulia) akiwa na Viongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni.





No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages