LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 26, 2021

MAMBO YA CHANJO UVIKO 19 YAWA GUMZO KONGAMANO LA WIKI YA AZAKI DODOMA+video

MAMBO ya Chanjo ya UVIKO-19 amekuwa moja ya mijadala katika Kongamano la Wiki ya Azaki lililofanyika leo kwenye Ukumbi wa Royal Village jijini Dodoma, Miongoni mwa waliochangia mjadala wa UVIKO 19 ni Kiongozi wa Chama cha Wazalendo (ACT), Zitto Kabwe na wadau wa Asasi za kiraia ambapo wengi wao wameshauri elimu kuhusu chanjo ya UVIKO 19 itolewe hadi vijijini.
Jopo la  viongozi wa asasi za kiraia wakiwa meza kuu wakati wa kongamano tayari kufafanua na kujibu maswali kutoka kwa wadau.

Katibu wa Chama cha Viziwi Tanzania, Wilaya ya  Korogwe,Allz Nassoro akitoa maoni yake na kutaka watu wenye ulemavu wa aina hiyo kuwashirikisha kupata elimu ya chanjo ya UVIKO-19.
Mtaalamu kutoka UNICEF, Alex Mphuru akijibu baadhi ya hoja kuhusu mambo ya UVIKO -19.
Mkurugenzi kutoka Taasisi ya Family Hearth International  (Fhi360),Dkt Beatees Leon  akijibu maswali ya wadau kuhusu UVIKO 19.
Baadhi ya wadau wa asasi za kiraia wakisikiliza kwa makini kusikiliza wakati wa kongamano hilo.

 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza  kupitia clip hii ya video wadau wakitoa maoni yao na kupata majibu wakati wa kongamano hilo......

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages