LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 29, 2021

WAZIRI GWAJIMA AVUTIWA NA TAASISI YA T-MARC TAMASHA LA KARIBU DODOMA FESTIVAL 2021

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, DKT Dorothy Gwajima,  akipokea zawadi kutoka kwa  Mwakilishi wa Mauzo wa Taasisi ya T-Marc Tanzania alipotembelea banda la Taasisi hiyo kwenye maonesho ya Karibu Dodoma Festival 2021 katika viwanja vya Chinangali Park, Jijini Dodoma.

T-MARC Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali ambalo limejikitakatika kuboresha masuala ya afya katika kijamii. 

 Ina bidhaa zenye viwango vya juu na zinazouzwa kwa bei nzuri  sambamba na programu mbalimbali zinazo elemisha jamii juu ya masuala ya afya ya upangaji  wa uzazi na afya ya uzazi kwa ujumla.

Aidha, T-MARC  hujishughulisha pia na maisha ya mtoto, maji na usafi wa mazingira, lishe na magonjwa ya kuambukiza/yasiyo ya kuambukiza kama vile malaria, VVU/UKIMWI na saratani ya shingo ya kizazi. Tovuti yetu ni (www.tmarc.or.tz)


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages