LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 29, 2021

IKULU: RAIS SAMIA KWENDA SCOTLAND KESHO, NI KATIKA MKUTANO WA COP 26

Ikulu, Dar es Salaam

Rais  Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuondoka nchini kesho, kwenda Glasgow, Scotland kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26).


Taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jackson Msangula, Jijini Dar es Salaam,  imesema, Rais Samia anatarajiwa kuhutubia mkutano huo, Novemba 2, 2021 ambayo itakuwa siku ya pili ya Mkutano huo wa COP 26. 


Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Rais Samia anatarajiwa pia kukutana na kuzungumza na baadhi Wakuu wa nchi, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa Taasisi mbalimbali pamoja wafanyabiashara wakubwa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi hizo na Taasisi zao.


"Lengo la Mkutano huo wa COP 26 ni kujadili jitihada za kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa ili kupunguza joto duniani", imesema taarifa hiyo.

Rais Samia Suluhu Hassan

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages