Mtandao wa wanawake wa dini mbalimbali katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini wameiomba Serikali kufanya marekebisho ya sheria zinazochochea ukatili wa kijinsia ikiwemo masuala ya mirathi na ndoa za utotoni.
Wameyasema hayo walipokutana mjini Moshi katika mkutano ulioandaliwa na makao makuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (ELCT), Dayosisi ya Kaskazini kwa ushirikiano na Norwegian Church Aid Tanzania.
Mwenyekiti wa wanawake wa dini ya kiisalmu mkoani Kilimanjaro, Zawia Massawe amesema ni wakati sasa Serikali kupitia wizara husika kuona umuhimu wa kufanya marekebisho hayo ya kisheria zinazokandamiza haki za kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike.
“Kuna vitu vinachochea ukatili wa kijinsia kwenye jamii zetu ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa baadhi ya sheria zisizo rafiki katika kudhibiti vitendo hivi na zinapaswa kutazamwa upya, tunaomba Serikali iangalie hili kwa jicho pana,” amesema
Pamoja na mambo mengine, Josephine Shoo ambaye ni kiongozi wa wanawake katika makanisa ya kipentekoste ameiomba Serikali kushirikiana na wadau wengine kutenga rasilimali za kutosha kuchangia mambo yanayohusu afya bora na usawa wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇