WAKAZI jijini hapa wametakiwa kujikita katika kilimo chenye tija kwani Tanzania imejaaliwa ardhi ya kutosha, na kuachana na ile dhana ya kwamba kilimo kinawafaa watu wasio na ajira pekee.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka wakati akifungua maonesho ya siku saba ya kilimo kanda ya kati yanayoendeshwa na Kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini (JATU PLC) yajulikanayo kama wiki ya mavuno.
Amesema Jamii hasa vijana wanadhani ya kwamba kilimo ni cha watu wasio na shughuli zingine za kufanya kitu ambacho si sahihi kwani wanaweza wakalima huku wakiwa ofisini au vyuoni wakiendelea na majukumu yao wakalima na kampuni ya JATU.
“Sisi kama Taifa Tumekuwa na uhaba wa mafuta kipindi kilichopita tukaja na mikakati ya kulima zao la alizeti kwenye mikoa mitatu ya Singida Dodoma na Simiyu kwa kuanza kuzalisha mbegu tani laki 5 kwaajili ya kuondokana na uhaba wa mafuta wakati huu ndio ulikuwa mzuri kuchangamkia fursa hizi”.amesema Mwanahamis
Na kuongeza kusema kuwa “Sasa kumbe tulikuwa tunawaza sawa sawa kama JATU mnavyowaza ifike mahala sasa tuwe na dhana ya nilime nijilishe na siyo tusubiri watu wengine walime na hutujui wanalima kwa aina gani mbegu gani wanatumia” amesema Mwanahamis
Kwa upande wake Meneja kutoka Taasisi ya JATU Mohamed Simbano amesema kampuni hiyo ilianzishwa na vijana wa kitanzania ambao ni wahitimu wa chuo kikuu cha Dar es salaam lengo likiwa ni kuhakikisha ustawi wa maisha ya watu kiafya kutokana na bidhaa bora na asilia zinazotokana na kampuni hiyo.
“Pia inatoa suluhisho katika kupunguza umasikini kwa kutumia ipasavyo rasilimali watu kilimo cha kisasa na shughuli za viwanda pamoja na kugawana faida na mlaji wa mwisho”amesema Simbano.
Akizungumzia kuhusu maonesho hayo amesema lengo la maonesho hayo ni kuweza kuhakikisha jamii kila mkoa wilaya hasa wakulima ambao wengi wapo katika mikoa mbalimbali na wengi wamekuwa wakiomba kampuni hiyo iweze kuwafikia.
“Lengo letu ni ili maeneo yote ili kujifunza namna ya kuimarisha na kuchochea ukuaji ukuwaji wa sekta ya kilimo kama ilivyo sera ya kilimo na mikakati ya serikali katika kuhimiza taasisi kuweka nguvu katika kilimo kwa kuwa ndo sekta inayochangia mkwa sehemu kubwa pato la taifa”
Hata hivyo maonesho hayo ya kilimo kanda ya kati yanatarajia kufungwa tarehe 20 october huku yakiwa yamebebwa na kauli mbiu isemayo wiki ya mavuno anza na ekari moja
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇