LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 15, 2021

SABAYA NA WENZAKE WAPATIKANA NA HATIA YA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA, WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA

Arusha, leo
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia katika kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo ambaye amesema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka dhidi ya Sabaya na wenzake na amewatia hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hakimu Omworo amesema, imethibitisha mshtakiwa wa kwanza (Sabaya) alikuwa na bastola ndani na nje kulikuwa na watu wawili wenye silaha hivyo, hakuna shaka duka la shahidi wa kwanza lilivamiwa na watu wenye silaha na lilikuwa chini ya watu wenye silaha.

Katika utetezi wake, Sabaya ameiomba mahakama imuonee huruma kwani sio yeye bali alikuwa anatekeleza maagizo ya Mamlaka yake ya uteuzi na ana mchumba walikuwa wafunge ndoa na mahali ameishalipa.

Baada ya washtakiwa kutiwa hatiani, Hakimu Amworo aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ndipo, wakili wa Serikali Wakili wa Serikali, Felix Kwetukia amesema hawana kumbukumbu ya makosa ya zamani ya washtakiwa wote watatu na wameiomba Mahakama iwape adhabu ya miaka isiyopungiua 30 jela na viboko.

Sabaya na wenzake walifikishwa mahakamani leo saa 3:05 asubuhi, kwa ajili ya hukumu ambapo Oktoba 1, 2021 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo kwa maelezo ya kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo, Sabaya alikuwa anatetewa na Wakili Moses Mahuna, Silvester Kahunduka na Wakili Fridolin Germelo.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wakiingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza Hukumu ya Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha. 

Chanzo: Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages