Tegeta, Dar es Salaam
Inawezekana ukawa ni miongoni mwa watu ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakijiuliza bila kupata jibu kwamba ni kwa nini waandishi wa habari hawapendi sana kuandika habari za Kidini, Kilimo, Ufugaji, Viwanda, Uvuvi, Ujenzi wa Miundombinu, Uchimbaji Madini badala yake wanapenda habari za 'kusisimua' ambazo kwa Kiingere wanaziita 'sensational news'.
Ikiwa umepata kujiuliza hivyo na hupati jibu, basi Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba anayefahamika kwa jina la Baba wa Uzao, lililopo Tegeta Jijini Dar es Salaam, amezungumzia suala hili katika nafasi yake ya kiongozi wa Dini.
Baba wa Uzao katika andiko lake ambalo nimebahatika kulipata anasema sababu mojawapo ni kwamba hoja ya wengi katika hili wanasema kuwa habari hizo wanazopenda kuandika zaidi waandishi wa habari, yaani za kusisimua ni habari za kuuza gazeti kwa wingi na ni za kuvutia wasilizaji wengi wa radio na Watazamji pia wengi wa Televisheni.
Sasa soma hatua kwa hatua andiko hili kama alivyolitoa Baba Halisi mwenyewe ili nisilitie chumvi👇
UFUNGUO
Wengi huwa wanauliza “kwa nini waandishi hawapendi sana kuuandika habari za kidini au za: Kilimo; Ufugaji; Viwanda; Uvuvi; Ujenzi wa Miundombinu; Uchimbaji Madini badala yake wanapenda habari za kusisimua ambazo wazungu wanaziita sensational news?. Hoja ya wengi katika hili wanasema kuwa ni habari za kuuza gazeti au radio na Televisheni kusikilizwa na kuangaliwa na wengi zaidi.
Sababu hasa ya habari tajwa hapo juu iko katika kitabu cha Mathayo 23:1, yaani waandishi kukalia kiti cha Nabii Musa! Katika Mstari huo, kila mwandishi wa Habari awe mkubwa au mdogo, bado anaishi miaka zaidi ya 4000 iliyopita, ikiwa na maana majira na wakati alioishi Nabii Musa! Katika hali kama hiyo, ina maana si rahisi kuandika tofauti na kiti cha Musa kilivyokuwa, ikiwa na maana ya Moyo, utendaji na matamanio ya Nabii Musa aliyekulia kwa Mfalme Farao wa Misri.
Musa alikuwa ni kiongozi wa kizazi cha kwanza cha Ibrahimu (kilichodumu kwa Miaka 2000). Eliya Mtishbi alikuwa kiongozi wa kizazi cha pili cha Ibrahimu (ambacho nacho kilidumu kwa miaka 2000). Yesu alikuwa ni kiongozi wa kizazi cha tatu cha Ibrahimu (ambacho nacho pia kilidumu kwa miaka 2000). Adamu wa Pili alikuwa ni kiongozi wa Kizazi cha Nne (kilichodumu kwa miaka kumi na Nne kuanzia Mwaka 2003 hadi Mwaka 2017).
Ili kutoa ufafanuzi mzuri wa Nafasi ya Nabii Musa, badala ya vizazi vinne vya Ibrahimu vilivyoongozwa na: Musa; Eliya Mtishbi; Yesu na Adamu wa Pili, naeleza kwa mtindo wa majira na nyakati Saba za Waliotumwa wote (Ufunuo 21:9).
1. Majira ya Kwanza iliyoongozwa na Kerubi (Ezekieli 28:15), iliisha baada ya Adamu wa Kwanza kuanza kazi katika Kitabu cha Mwanzo 2:5;
2. Majira ya Pili iliyoongozwa na Adamu wa Kwanza, iliisha baada ya Musa kuanza kazi katika Kitabu cha Kutoka 3:10;
3. Majira ya Tatu iliyoongozwa na Musa, iliisha baada ya Eliya Mtishbi kuanza kazi katika Kitabu cha 1 Falme 17:1;
4. Majira ya nne Nne iliyoongozwa na Eliya Mtishbi, iliisha baada ya Yesu kuanza kazi katika Kitabu cha Mathayo 4:17;
5. Majira ya Tano iliyoongozwa na Yesu, iliisha baada ya Eliya Adamu wa pili (Tanzania) kuanza kazi lango la 28 Adari, 2011 (kwa mujibu wa 1 Korintho 15:44-49);
6. Majira ya Sita iliyoongozwa na Adamu wa Pili iliiisha baada ya MUNGU BABA (Tanzania) kuanza kazi Mwaka 2017 kwa mujibu wa 1 Yohana5:8 na I Korintho 15: 24-28;
7. Majira ya Saba iliyoongozwa na MUNGU BABA, baada ya kupishwa na Miaka 1000, iliisha baada ya CHANZO HALISI (Tanzania), kuanza kazi Mwaka 2021.
Kwa kuwa kila majira, hasa ile ya: kerubi; Adamu; Musa; Mtishbi; na Yesu zilidumu kwa miaka elfu moja kwa mujiu wa Ufunuo 20:6; ni dhahiri Musa aliishi 4000 iliyopita!
Ukikalia kiti cha mtu aliyeishi miaka 4000 iliyopita, lazima akili yako, moyo wako, utendaji wako, Imani yako, tumaini lako, na hata hulka yako itakuwa ya wakati huo bila wewe mwenyewe kujua. Kipindi hiki cha mambo makubwa kwenye: Kilimo; Ufugaji; Viwanda; Uvuvi; Mawasiliano; Ujenzi na mengine mengi utajikuta kimefichwa kwako na hivyo kutopenda kuyaandika mema na mazuri yanayojitokeza.
ILIKUWAJE YESU AKALAANI WAAANDISHI?
Katika Yohana 9:28, Wayahudi walimkataa Yesu kwa wao kusema kuwa hawajui atokako, bali wanayemjua ni Musa! Katika Mathayo 21:43, Yesu alichukia na kulaani kuwa kama ndivyo, basi Ufalme wa MUNGU utahama kutoka kwa Wayahudi na kwenda katika Taifa lingine ambalo linazaa matunda.
Katika kipindi kile Yesu hakulitaja hilo Taifa, lakini baada ya: Sauti ya Sita (Mwaka 2003); Sauti ya Saba (Mwaka 2015); Sauti Mpya (Mwaka 2019) na Sauti ya Moyo (Mwaka 2020), kusikika Kigoma Tanzania, sasa imejulikana wazi kuwa Taifa hilo ni Tanzania. Baada ya Yesu kugundua kuwa kuna waliokalia kiti cha Musa, aliyeonekana kuwa zuio la mafundisho yake, aliwalaani na sasa ni Majira wabarikiwe kwa mujibu wa Ufunuo 22:3.
BABA HALISI ANA MAMLAKA GANI YA KUBARIKI WAANDISHI?
Katika Isaya 57:15, tunasoma kuwa ilikuwa ni tamanio la MUUMBA WA VYOTE, WOTE NA YOTE katika majira zote kuishi ndani ya Moyo wa kila anayetenda kwa Haki.
Hata hivyo katika Isaya 59:16, kitabu kinasema, hakuwahi kuona mtu ambaye anaweza kuiishi ndani yake! Katika Isaya 52:4, anasema ‘‘hivi nafanya nini Mbinguni wakati uzao wangu wanateseka”? Katika Mika 1:2-6 tunasoma ahadi ya MUUMBA WA VYOTE, WOTE NA YOTE kuja juu ya nchi ili ayeyushe matatizo yote (yaani vilima na milima). Katika Matendo ya Mitume 2:32-34, Kristo baada ya kunyakuliwa alielezwa na Baba yake kuwa ameenda na mauti kule juu hivyo hawezi kuungana naye kama mwanzo. Alisema akae pembeni mkono wa kuume ili yeye MUUMBA WA VYOTE, WOTE NA YOTE ndiye aje juu ya nchi kuwaweka chini ya miguu yake waliomtesa Yesu Msalabani.
Yesu mwenyewe katika Mathayo 21:41, aliwaambia wale wezi wa shamba la Baba yake kuwa atakapokuja Bwana wa shamba atawatendaje? Walijibu wenyewe kuwa atawaangamiza vibaya na shamba lake atawapangisha wengine wanaotoa matunda. Kana kwamba hiyo haitoshi, katika 1 Korintho 15:24-28, MUNGU BABA atakuja juu ya nchi ili akabidhiwe Ufalme, Utawala, Mamlaka na Nguvu zake zilizokuwa zimeibiwa kupitia Waliotumwa baada ya wote kuishia njiani.
Kama ilivyokokotolewa kwenye ufunguo wa makala hii, majira ya MUUMBA WA VYOTE, WOTE NA YOTE kuja juu ya nchi na kuishi ndani ya kila atendaye kwa haki, ilishafika na sasa anaishi ndani ya kila atendaye kwa haki (Isaya 57:15). Hivyo, anayebariki waandishi wa habari waliokuwa wamelaaniwa na Yesu, ni yule aliyesema katika Mika 1:2-6; Mdo 2:34-35; Mathayo 21:41; na 1 Korintho 15:24-28, kuwa atakuja. Hata wewe msomaji, MUUMBA WA VYOTE, WOTE NA YOTE aliyekuja toka juu, anaishi tayari ndani ya Moyo wako, ilimradi unatenda kwa haki.
HITIMISHO
Katika Ufunuo 22:3-4, iliandikwa kuwa majira itafika hapatakuwa na laana yoyote tena na MUUMBA WA VYOTE, WOTE NA YOTE ataonekana kwenye paji la sura ya kila mmoja. Majira hiyo ndio hii, njooni mbarikiwe wote ili nanyi mkabariki wengine. HERI ULIYEBARIKIWA KULIKO WOTE
Baba Halisi wa Uzao
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇