Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, leo imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kuwakomboa Wanawake kiuchumi, kwa kuwakutanisha Wanawake zaidi ya 200 wenye ulemavu kutoka mkoa huo na kuwanoa kwa semina ya Ujasiriamali.
Akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga, amesema Semina hiyo ni mwendelezo wa semina mbalimbali ambazo UWT mkoa huo imekuwa ikizitoa kwa nyakati tofauti, lengo likiwa ni kumwinua mwanamke kiuchumi.
Masunga amesema, ili kuiunga mkono katika dhamira yake hiyo, Wazazi wote wenye watoto walemavu wasiwafiche majumbani badala yake wawatoe ili wachanganyike na wenzao ili kuweza kuingizwa katika makundi ya wenzao katika kuwawezesha kujitegemea.
"Walemavu wanao uwezo kama nilivyo mimi, wanaweza kufanya kila jambo linaloweza kufanywa na asiye mlemavu, kwa hiyo nina wasihi sana wazazi wenye watoto wenye ulamavu msiwafiche majumbani watoto wenu, watoeni nje wachangamane na jamii ili nao wasaidie kujisaidia", amesema Masunga
Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Angel Akilimali, amewataka wenye ulemavu kusikia kuwa ni watu kama watu wengine na ulemavu walio nao ni uumbaji wa Mungu lakini ubinadamu wao ni sawa na walio nao wengine.
Amesema, Wenye ulemavu wajisikie wapo huru na salama kwa kuwa wako chini ya mikono salama ya Rais Samia Suluhu Hassa, ambaye kutokana na kuwajali ameendelea kuwawekea walemavu hao fursa mbalimbali ikiwemo mikopo isiyo na riba ambayo hutolewa na serikali kupitia Halmashauri zake nchini kote.
Akilimali aliwahimiza wenye ulemavu kutojiweka nyuma katika kuwania uongozi ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hivyo kuwhimiza kujitokeza kuomba nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa ndani ya CCM utakaofanyika mwakani.
Picha Mbalimbali za Semina hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni rasmi kufungua Semina ya Ujasiriamali kwa wenye ulemavu, iliyofanyika leo Ukonga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Anna Matinde Mkurugenzi wa Taasisi ya TASWE iliyodhamini Semina hiyo. Watatu ni Mgeni Rasmi Mjumbe wa NEC, Anjel Akilimali na anayefuata ni Katibi wa UWT mkoa huo Grace Haule na Diwani Aidan Amos wa Kata ya Kipawa ilikofanyika Semina hiyo.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akisisitiza jambo wakati akimshukuru Mkurugenzi wa Taswe (kushoto) kwa kufadhili Semina hiyo.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akimkabidhi kinasa sauti Mgeni Rasmi Angel Akilimali ili azungumze na kufungua Semina hiyo.Kisha meza kuu wakasimama wote kuimba wimbo maarufu wa 'Wanawake na Maendeleo' kumtayarisha Mgeni Rasmi kuzungumza.Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Angel Akilimali akizungumza kabla ya kuzindua rasmi Semina hiyo.Katibu wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Grace Haule alipokuwa akizungumza kufanya utambulisho mwanzoni mwa hafla hiyo ya Semina.Mkurugenzi wa Taasisi ya Taswe Anna Matinde akizungumza machache baada ya kukabiribishwa na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule.Diwani wa Kipawa Aidan Amos akizungumza machache baada ya kukabiribishwa na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule.Mbunge wa Viti Maalum kupitia Wenye Ulemavu Ikupa Stella Alex, akizungumza machache baada ya kukabiribishwa na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule.Chini, ni washiriki wa Semina hiyo wakiwa katika muonekano mbalimbali ukumbini👇
Kisha Shangwe Ukumbini baada ya semina kufunguliwa👇
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga kutokana na furaha aliyokuwa nayo akatamani kumwinua Mbunge Ikupa ili wacheze kidogo, lakini haikuwezekana kutokana na hali ya Mbunge huyo, ikabidhi wacheze akiwa ameketi. Wakaendelea kufurahi👇Sakata la wimbo wa 'Wanawake na Maendeleo likaendelea'👇
Ends: ©2021 CCM Blog/Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇