Na Alfred Mgweno (TEMESA)
Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) imetenga jumla ya shilingi bilioni 21.4 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vivuko vipya vitano kwa mwaka huu wa fedha 2021/2022 ambavyo vitatoa huduma katika maeneo mbalimbali ya mito, maziwa na bahari nchini.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa Ujenzi na Matengenezo ya Vivuko kutoka TEMESA Mhandisi Lukombe King'ombe wakati akizungumza na waandishi wa Habari kutoka Televisheni ya Taifa (TBC) waliofanya naye mahojiano Mkoani Mwanza katika kipindi maalumu cha Mulika ursa ambacho kinaangazia miradi yote ya Serikali iliyofanyika na ambayo inatarajiwa kufanywa na Serikali kwa mwaka huu wafedha.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇