LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 21, 2021

MBUNGE KILAVE, MADIWANI JIMBO LA TEMEKE WAISHUKURU SERIKALI YA RAIS SAMIA KWA KULISHIKA MKONO JIMBO HILO KIMAENDELEO

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog Temeke
Mbunge wa Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam Dorothy Kilave na Madiwani wenzake wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulishika mkono Jimbo hilo kimaendeleo ikiwemo kutengwa Sh. Milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Makangarawe kupitia Bunge la Bajeti lililopita.

Pia wameishukuru Serikali hiyo inayoongozwa na Rais Samia kwa kutengwa fedha kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kupatikana vifaa tiba kwenye Vituo vya Afya vya Buza na Malawi Cargo, Yombo Vituka,  jimboni humo.

Pongezi na shukrani hizo zimetolewa jana na Mbunge Kilave na Madiwani wa Kata 13 zililizopo katika Jimbo la Temeke na wa watatu wa Viti maalum, katika kikao maalum kilichoitishwa na Mbunge Kilave na kufanyika katika Ukumbi wa TCC Club, kwa ajili ya kutoa mrejesho wa mambo mbalimbali yaliyojiri katika Bunge la Bajeti ambalo lilihitimishwa mwezi Juni na Mkutano wa Nne wa Bunge uliohitimishwa Septemba 10, 2021, Jijini Dodoma.

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa pia na Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilayani humo Juma Ng'ombe kwa niaba ya Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke, Mbunge Kilave alieleza namna alivyotekeleza kikamilifu jukumu lake la kuwawakilisha Wananchi wenzake wa Jimbo la Temeke katika Bunge hilo la Bajeti lililohitimishwa mwezi Juni na Mkutano huo wa Nne wa Bunge.

"Ndugu zangu nikiwa Mbunge wenu na kiongozi mwenzenu ambaye nawakilisha wananchi wa Jimbo hili katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo nimewaita hapaa, kwanza kuwashukuru na kuwapongeza ninyi Madiwani kwa kazi kubwa mliyofanya ya kupigania kura zenu na Ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 na hatimaye nikaibuka mshindi wa Ubunge kupitia chama chetu pendwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pili, kikao hiki ni kikao tendaji ambacho ninadhamiria tushirikiane kwa baadhi ya mambo kadhaa ambayo ni sehemu ya utendaji wetu  na wajibu sisi Viongozi wawakilishi wa Wananchi kutoka katika kila Kata kwa maslahi na maendeleo ya Jimbo la Temeke", alisema Mbunge Kilave mwanzoni mwa kikao hicho na kuongeza;

"Kwanza, Kikao hiki kitakuwa na ajenda mbili, nahitaji nitoe mrejesho wa kilichojiri katika Bunge la Bajeti ambalo lilihitimishwa mwezi Juni na Mkutano wa Nne ambao tumehitimisha Seotemba 10, 2021. Pili, Nitapokea na kuweka Mikakati ya Pamoja katika Utendaji na kufanyika kazi kero za Wananchi".

"Bunge la Bajeti Wabunge nikiwemo mimi tulishiriki vyema na tukahitimisha kwa kupitisha Bajeti hiyo ya Serikali kwa asilimia 94 (kura 361), bajeti hii kupitia ile mipango ya Jumla imelenga kuinua Uchumi wa Wananchi na taifa kwa Ujumla, kwa kiwango kikubwa imelenga huduma za Jamii lama Ilani yetu ya Uchaguzi inavyoelekeza", alifafanua Mbunge Kilave katika Hotuba yake kwa Madiwani hao.

Alisema, kwa upande wa Jimbo la Temeke aliwasilisha Bungeni changamoto ya kutokuwa na Shule za Sekondari kwa baadhi ya Kata, kama kata za Chang'ombe na Makangarawe ambapo kupitia Bunge la Bajeti  kwa kuzingatia vigezo kadhaa kiasi hicho cha fedha cha Sh. milioni 600 kimetengwa  kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ya Sekondari ya Makangarawe.

Mbunge Kilave aliwambia Madiwani hao kuwa katika Suala la Miundombini aliwasilisha Bungeni Changamoto ya uchakavu wa Barabara  za Mitaa na kwamba tatizo kubwa lilikuwa ni bajeti ndogo katika Mamlaka ya TARURA inayohusika na barabara hizo, lakini sasa Serikali imetoa  fungu maalum la Sh. Milioni 500 kwa kila jimbo kwa ajili ya Ukarabati kwa baadhi ya barabara za mitaa.

Alisema, katika Jimbo la Temeke fedha hizo (Sh. milioni 500) walizigawa katika matengenezo ya Barabara tatu kwa kuzingatia vigezo vya Wizara, na kuongeza kuwa alijitahidi kushirikiana na Wataalam wa TARURA na kuteua Barabara mbili zilizopo Kata ya Tandika za Mvumero (Sh. Milioni 180) na Ngomano (Sh. Milioni 150) na ya tatu Barabara ya Keko iliyopo Kata ya Miburani (Sh. Milioni 170).

"Kutokana na Jitihada za kumtafuta Waziri na kueleza kazi kubwa inayofanywa na Wananchi wa Temeke katika kuchangia Uchumi wa Nchi kwa kuangalia Idadi ya Watu wake na Uhitaji, mikamuomba Waziri ikiwezekana tupate fungu jingine na kutokana na kuwa na vigezo vya kutosha Jimbo letu liliongezewa tena kiasi cha Sh. milioni 500", alisema Mbunge Kilave na kufafanua kuwa si kila jimbo lilipewa nyongeza hiyo.

Alisema, katika kiasi hicho cha awamu ya pili  walitumia vigezo vilevile  vya awali na kutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara tatu (3) alizozitaja kuwa ni Basra ya Chang'ombe (Sh. milioni 150,000), Amani Buza Kusini ya Buza (Sh milioni 245) na ya Keko B Rehmenj iliyopo Keko ( Sh. milioni 105).

Baadaye Mbunge Kilave aliwaambia Madiwani hao mambo mengine ambayo Mkutano wa Nne wa Bunge  lililoisha Septemba 10, 2021 na kisha akawaomba madiwani kutoa ushauri ili wajadilina nao kwa pamoja katika kikao hicho ili kuweka mikakati ya pamoja katika utendaji na kutatua kero za wananchi.

 

Aidha Mbunge Kilave aliwasilisha katika kikao hicho Mwongozo wa mpango wake kapmeni ya kuimarisha Usafi katika Jimbo hilo ambao ameupa jina la 'Fagio la Mama Kilave'.

Mbunge Kilave aliwasilisha mpango huo ili uajdiliwe na Madiwani hao ili kuuboresha kwa kutoa mapendekezo watakayoona yanafaa kuongezwa au kupunguzwa ili utakapozinduliwa katika siku wakatayokubaliana uweze kuwa na manufaa katika dhana nzima ya kulifanya Jimbo la Temeke liwe na usafi wa mazingira ulio endelevu.

Aliwaambia Madiwani kuwa ameamua kuibuka na mpango huo, kufuatia ziara mbalimbali alizofanya jimboni na kubaini kuwa maeneo mengi yamekithiri kwa uchafu na uchafuzi wa mazingira, jambo nambalo ni hatari kwa afya za wananchi na pia kulikoshesha mvuto jimbo kimazingira.

"Katika ziara zangu nilibaini kuwa kuna changamoto kubwa ya usafi wa mazingira, na hali hii imejidhihirisha katika maeneo ya Masoko, Vituo vya Mabasi, Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali, Mitaro na mifereji ya barabara, Maeneo ya wazi, mitaa nakadhalika.

Kutokana na Uchafuzi huu wa Mazingira, Ofisi ya Mbunge Jimbo la Temeke chini ya Idara ya Mazingira imeandaa Kampeni kwa jina la FAGIO LA MAMA KILAVE ambayo ni shirikishi kwa wananchi katika kufanya usafi wa mazingira ndani ya Jimbo la Temeke ili kuboresha kuboresha usafi wa mazingira katika Jimbo letu", alisema Mbunge Kilave na kusambaza nakala za mwongozo huo kwa madiwani ili wausome kwa kina kabla ya kujadili.

Akizunguza kwenye Kikao hicho, Meya wa Manispaa ya Temeke  Menya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika ambaye baadaye hakushiriki madajiliano kutokana na nafasi yake, aliupongeza mpango huo na kuahidi kuunga mkono huku akiwashawishi madiwani wenzake nao kuunga mkono ambapo walikubaliana naye.

"Waheshimiwa Madiwani, Nawasalimia kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", Mbuge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akisalimia mwanzoni mwa kikao chake na madiwani wa Kata 13 za jimbo hilo, kilichofanyika TCC Club, Temeke jijini Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kibonde Maji Jimbo, Mbagala na kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Temeke Juma Ng'ombe.
Katubu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Temeke Juma Ng'ombe (aliyesimama), akizungumza katika Kikao hicho kumwakilisha Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo.
Mbuge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akisoma katika kikao hicho, Taarifa yake ya mrejesho wa mambo mbalimbali yaliyojiri katika Bunge la Bajeti ambalo lilihitimishwa mwezi Juni na Mkutano wa Nne wa Bunge uliohitimishwa Septemba 10, 2021, Jijini Dodoma.
Mbuge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akifafanua jambo bada ya kusoma katika kikao hicho, Taarifa yake ya mrejesho wa mambo mbalimbali yaliyojiri katika Bunge la Bajeti ambalo lilihitimishwa mwezi Juni na Mkutano wa Nne wa Bunge uliohitimishwa Septemba 10, 2021, Jijini Dodoma. Kulia ni baadhi ya Madiwani wakimsikiliza kwa makini.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Wilaya ya Temeke Juma Ng'ombe (kulia) akinukuu kwa makini, wakati
Mbuge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akiwasilisha katika kikao hicho, Taarifa yake ya mrejesho wa mambo mbalimbali yaliyojiri katika Bunge la Bajeti ambalo lilihitimishwa mwezi Juni na Mkutano wa Nne wa Bunge uliohitimishwa Septemba 10, 2021, Jijini Dodoma.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Temeke Mathias Jonas alipokuwa akisoma ajenda za kikao hicho.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kibonde Maji Jimbo, Mbagala akizungumza katika kikao hicho huku Mbunge  Kilave akimsikiliza kwa makini. Meya huyo aliwaasa Madiwani kupendana na pia kuacha kusemana vibaya na kutoa maoni ya kikazi mitandaoni badala yake watumie vikao vya Chama au kama hiki alichoitisha Mbunge Kilave.
Mbunge Kilave na Meya Mtinika wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mapumziko kabla ya kujerea umbumbini kuanza mjadala wa mambo mbalimbali kuhusu Jimbo la Temeke.
Mbunge Kilave akizungumza jambo la Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania wilaya ya Temeke Ndugu Ng'ombe wakati wakirejea ukumbini baada ya picha ya pamoja.
Mbunge Kilave akijadiliana jambo na kuagana na Meya wa Temeke Ndugu Mtinika kabla ya Meya huyo kuondoka baada ya sehemu ya kwanza ya kikao hicho.
Maafisa kutoka Ofisi ya Mbunge Dada Hope (kulia) na Mwenzake, wakifurahia jambo, wakiwa nje ya ukumbi wakati wa mapmziko ya kikao hicho.  

"Mwanya, tunashukuru Kikao cha Mheshimiwa Mbunge wetu Dorothy kinaenda vizuri", wakasema.

©2021 CCM Blog/Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages