Rais Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa viongozi wa kitaifa wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) alioufungua jijini Dodoma Septemba 27,2021.Wadhamini wakuu wa mkutano huo ni Benki ya NMB. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe akizungumza kwa lengo la kuwakaribisha wajumbe wa mkutano mkuu maalumu jijini humo. |
Baadhi ya viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma wakihudhuria mkutano huo.
Mbunge wa Sumbawanga, Aesh Hillary (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Kyela, Ali Jumbe Mlagila wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akizungumza jambo na maofisa wa Benki ya NMB wakati wa mkutano huo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Fatma Mganga (kulia) akijadiliana jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna.
Rais Samia na viongozi wengine wakipiga makofi baada ya kumalizika kwa wimbo wa Taifa.
Rais Samia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge
Rais Samia akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa mkutano huo.
Rais Samia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madiwani kutoka wilaya za mkoa wa Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalumu, Dkt. Pindi Chana (kulia) akiwa na baadhi ya wabunge wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda (kulia) akijadiliana jambo na Mbunge wa Chemba, Mohamed Moni pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu, Ritha Kabati.Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu nchini (TEA), Bahati Geuzye, akizungumza na waandishi wa habari, mazungumzo hayo yalifanyika katika banda la mamlaka hiyo lililokuwa katika mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Viongozi wa Alat Taifa uliofunguliwa na Rais Salia Suluhu Hassan jijini Dodoma juzi.
Na Mwandishi Maalumu Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitaka Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuimarisha usimamizi na udhibiti wa fedha za Serikali ili ziweze kutumika vizuri na kuleta tija katika miradi ya kimkakati na kuwaletea wananchi maendeleo.
Mhe. Rais Samia asema hayo leo tarehe 27 Septemba, 2021 wakati akifungua Mkutano Maalum wa Uchaguzi wa viongozi wa ALAT uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Aidha, Mhe. Rais Samia ametaka kuimarishwa kwa ukusanyaji wa mapato kwa kutumia TEHAMA na kubuni vyanzo vipya vya mapato bila kutumia mabavu katika kukusanya tozo na ushuru.
Pia Mhe. Rais Samia amewaagiza viongozi wa ALAT kuchukua hatua kwa watendaji wote watakaobainika kufanya ubadhirifu ili tija ionekane katika miradi ya maendeleo na kwenye fedha za mikopo ya asilimia 10 zinazotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Aidha, Mhe. Rais Samia ameitaka ALAT na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwashirikisha wananchi katika kuandaa miradi ya maendeleo ya kimkakati kwani baadhi ya miradi imeshindwa kufikia malengo kutokana na ushirikishwaji mdogo ama kutoshirikishwa kwa wananchi.
Mhe. Rais Samia ametolea mfano wa baadhi ya miradi kama masoko na stendi kujengwa katika maeneo ambayo wananchi hawafiki na hivyo kutelekezwa au kutumika kwa kusuasua.
Vilevile, Mhe. Rais Samia ameitaka Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuhakikisha inapoandaa mipango ya maendeleo inazingatia Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao ni wa mwisho katika kutekeleza dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025.
Mhe. Rais Samia ametoa wito kwa Viongozi wa Mikoa, Wilaya, Halmashauri, Kata na vijiji kutenga siku maalum kila wiki kusikiliza na kutatua kero za wananchi, zikiwemo za mirathi na migogoro ya ardhi, ambazo zimekithiri nchini.
Pia Mhe. Rais Samia amebainisha kuwa kwa sasa kipaumbele kikubwa katika Serikali ya Awamu ya Sita ni kujenga vituo vya afya kwa Tarafa 250, upatikanaji wa maji safi na salama, ujenzi wa barabara pamoja na madarasa.
Kuhusu Ujenzi wa madarasa, Mhe. Rais Samia amesema alilelekeza fedha za Tozo ziende kujenga vituo vya afya na madarasa lakini sasa amepata fedha mahali ambazo zitajenga jumla ya madarasa 15,000 na kuwezesha watoto wote wanaostahili kuanza shule mwezi Januari mwaka 2022 kupata fursa hiyo.
Aidha, Mhe. Rais Samia amewataka Mameya, Wenyeviti, Madiwani na watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kushirikiana na kuacha migogoro kati yao kwasababu tabia hiyo inazorotesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuharibu taswira ya Serikali kwa jamii.
Mhe. Rais amewataka viongozi wa mikoa kuendesha kampeni ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki zoezi la kuchanja kwa hiyari ili kujikinga na UVIKO 19, kwa kuwa ugonjwa huo bado ni tishio.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇